Wananchi Yanga
Stori

Yanga Yaitwa Malawi

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imepokea mualiko kutoka serikali ya Malawi kwenda kucheza mchezo maalum katika siku ya kuadhimisha Uhuru wa nchi hiyo.

Akiongea mbele ya Waandishi wa habari Afisa habari wa klabu ya Yanga Ally Kamwe amesema “Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Ni heshima kubwa sana kwa Klabu yetu na kwa Taifa kwa ujumla,” alisema Ally na kuongeza

“Mgeni wa heshima kwenye sikukuu za uhuru wa Malawi ni Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali ya Malawi ikatupa heshima hii ya kipekee kwa mualiko huu mkubwa na wa kihistoria” 

Ali Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga akiongea mbele ya Waandishi wa habari.

Kuelekea katika mchezo huo tayari uongozi wa Yanga umeshawaita wachezaji wao waliokua mapumzikoni na wataondoka nchini hivi karibuni kuelekea mchezo huo na watakwenda Malawi kwa ndege maalum.

“Napenda kutoa shukrani na pongezi kwa wachezaji wetu ambao watatoka mapumzikoni na kuungana nasi kwenda kuiwakilisha Nchi na Klabu yetu kwenye mualiko huu mkubwa. Tunatarajia kuondoka siku ya Jumatano na kama kawaida yetu ndege maalum kabisa itatupeleka Malawi na kutusubiri kisha tutarejea Dar es Salaam siku ya Alhamisi baada ya sherehe hizo,” alisema Kamwe.

Yanga itaondoka nchini July 5 na ikiwa huko itacheza na klabu kongwe na yenye mafanikio nchini Malawi Nyasa Big Bullets

Sambaza....