Yondani akiwahi mpira kuuzuia..
BlogTetesi

Yondani kurudishwa Yanga

Sambaza....

Taarifa mpya ni kuwa beki mkongwe Kelvin Yondani anaweza kurejeshwa kikosini baada ya kuanza mazungumzo mpya na uongozi wa Yanga

Yondani na Juma Abdul walikuwa katika mpango wa kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao hata hivyo wachezaji hao waligomea ofa walizopewa awali na hivyo kuruhusiwa wakatafute changamoto mahali pengine

Inaelezwa Yondani amefungua mazungumzo mapya na mabosi wa Yanga hivyo upo uwezekano anaweza kurejeshwa kundini

Bado siku nane tu dirisha la usajili linafungwa, na inavyoonekana wakongwe hao hawajapata ofa nono zaidi ya zile walizokuwa wamepewa na Yanga

Mcongomani Papy Tshishimbi nae inaelezwa aliwaangukia viongozi wa Yanga akiwa tayari kusaini mkataba aliokuwa amepewa awali

Hata hivyo ujio wa Mukoko Tonombe umefuta rasmi uwezekano wa nahodha huyo wa zamani kufikiriwa upya

Tshishimbi tayari ameondoka nchini kurejea kwao Congo, baada ya kutoswa ma klabu ya Simba aliyokuwa akiitumia kutaka dau kubwa Yanga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.