Ligi Kuu

Zahera alitudanganya kwa Kindoki, bado anaendelea kwa Molinga

Sambaza....

Kila jua linapochomoza kuna vitu vingi sana vya kujifunza. Jua huchomoza na kurasa nyingi sana za mafundisho katika maisha ya mwanadamu yoyote yule.

Mafundisho ndiyo chakula cha ubongo kwa mwanadamu yoyote yule. Maisha hayawezi kudhubutu kupiga hatua ya kusogea mbele bila kujifunza.

Kujifunza ambako kunahitaji uvumilivu, usikivu wa hali ya juu. Hutakiwi kuwa na mambo mengi unapojifunza. Unatakiwa kuwa mvumilivu na msikivu kupita kiasi.

Kwenye usikivu kuna darasa jipya. Darasa ambalo huimarisha na kubomoa. Darasa hili huimarisha kipindi unapopata elimu stahiki na yenye nguvu kubwa.

Kubomoka huja kipindi ambacho unapata elimu ambayo haina uhalisia. Ndioo hapo Jakaya Mrisho Kikwete alipowahi kusema akili ya kuambiwa changanya na za kwako.

Usiamini kila kitu unachokisikia au kuambiwa. Jipe muda wa kutafakari na kuja na kitu sahihi ambacho kinakupa nafasi kubwa ya uhalisia wa kitu unachokiona.

Zahera

Mara nyingi kutafakari ndiko kunakupa jibu sahihi kwenye maisha yako. Kuna mengi sikio langu lishayasikia sana kutoka kwa kocha Mwinyi Zahera. Mengi yana ukweli mengine hayana ukweli ukikaa ukayafikiria vyema.

Mwinyi Zahera aliwahi kuniaminisha kuwa Klaus Kindoki ni kipa bora kabisa wa kiwango cha juu, nilitulia nikajipa muda mwingi wa kutafakari na kumfuatilia Klaus Kindoki.

Mwanzoni alianza kunipa majibu tofauti na maneno ya Mwinyi Zahera, niliona Mwinyi Zahera ananidanganya. Nikampa muda tena Klaus Kindoki lakini hakuna alichokuja kunionesha zaidi ya makosa yake mengi binafsi.

Leo hii Yanga ina David Molinga. Huu ni usajili wa Mwinyi Zahera na ni usajili ambao Mwinyi Zahera amekuwa akituaminisha kuwa ni mshambuliaji bora zaidi.

Mshambuliaji ambaye alimpendekeza yeye kama yeye kwa kuamini katika miguu yake. Lakini kadri muda unavyozidi kwenda hakuna cha kutisha kwenye miguu mizito ya David Molinga.

Miguu iliyobeba mwili mzito , mwili ambao umebeba ubongo usio na ubunifu mkubwa kama washambuliaji wakubwa ambao washapita pale Yanga.

Amekuwa hana madhara makubwa kwa mabeki wa timu pinzani. Usajili huu utakuwa na hadithi tuliyoaminishwa kwa Klaus Kindoki ambaye tuliamishwa na kocha kuwa ni kipa bora


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.