ASFC

Zahera- Alliance ni timu ya kufungwa 5-0

Sambaza....

Yanga ilifanikiwa kuitoa Alliance School’s fc katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho, Azam Federation Cup kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya timu zote kutoka sare kwenye muda wa kawaida.

Akizungumza na mtandao huu wa Kandanda.co.tz kwenye mahojiano maalumu kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amedai kuwa Alliance School’s FC ilikuwa inatakiwa kufungwa 5-0.

Alizidi kusema kuwa jinsi ambavyo Alliance School’s FC wanavyocheza kunawapa nafasi kubwa ya kuadhibiwa, kwa sababu wachezaji sita huwa wanaenda kushambulia.

Yanga wakishangilia

Mwiñyi Zahera aliendelea kusema kuwa , timu inapoamua wachezaji sita waende kushambulia, nyuma huacha uwazi.

Uwazi ambao ukitumika vizuri kwa mashambulizi ya kushtukiza basi wanaweza kuadhibiwa sana.

Mwinyi Zahera amedai kuwa yeye hakufanikiwa kuwafunga goli hizo kwa sababu hakuwa na wachezaji wenye mbio ambao wangeweza kufanya mashambulizi ya kushitukiza.

Mwinyi Zahera aliongezea kuwa katika michezo ya mitoano kama hii ya Azam Federation Cup timu haitakiwi kufikiria kucheza vizuri . Timu inatakiwa kufikiria jinsi ya kupata matokeo. Ndicho kitu ambacho Alliance School’s FC wanatakiwa kujifunza.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.