Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi leo wamekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya Sportpesa Supercup baada ya kuifunga Afc Leopard ya Kenya kwa mabao mawili kwa moja.

Achana na kuanza kwa pamoja kwa mafundi Cleotus Chama na Haruna Niyonzima, leo alikua ni Zana Coulibaly alieishika Taifa kwa shughuli pevu aliyoionyesha.

Tazama hapa jinsi “move” ya bao la kwanza lilivyofungwa kutoka pasi ya kwanza kutoka kwa Haruna Niyonzima mpaka kwa Emmanuel Okwi alipofunga bao la kwanza la Simba leo.

Licha ya kutengeneza bao la kwanza la Emmanuel Okwi katika dakika za mwanzo leo Coulibaly alikua katika kiwango cha juu huku mara kwa mara mashabiki walikua wakimshangilia kutokana na kasi yake ya kupeleka mashambulizi.

Tazama jinsi goli lilivyofungwa kwa picha.


Sambaza....