Chirwa (Kushoto) na Hans (Kulia), kocha wa Azam FC sasa. Hapa ni wakati wote wakiwa Yanga.
TetesiUhamisho

Chirwa kutua Azam Fc

Sambaza....

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Obrey Chirwa inawezekana akatua katika klabu ya Azam FC. Taarifa za ndani zinasema kuwa mpaka sasa Obrey Chirwa ana nafasi kubwa ya kutua kwenye timu hiyo yenye makazi yake Chamanzi, Dar-es-Salaam.

Obrey Chirwa aliachana na Klabu ya Yanga mwishoni mwa msimu uliopita na kuamua kutimkia nchini Misri ambako hakuweza kufanikiwa kucheza kwa muda mrefu, tulimshuhudia akiwa Jukwaani msimu huu akiishuhudia timu yake ya zamani Yanga akiwa na baadhi ya viongozi wa Yanga.

Tutazidi kukupa taarifa zaidi kuhusiana na hizi habari za Obrey Chirwa kutua katika klabu ya Azam FC.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x