EPL

Tatizo linaanzia kwenye Kivuli cha Ferguson

Sambaza....

Alama yake aliitumia kuiweka kwa miaka 27, umri wa mtu mzima. Akili, nguvu na muda wake mwingi aliuwekeza katika maisha ya Manchester United.

Ndiyo maana alifanikiwa kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa sana katika klabu ya Manchester United

Alihakikisha kila sekunde inayopita katika maisha yake ilikuwa ni muhimu kuwapa furaha mashabiiki wa Manchester United.

Alifanikiwa kwa hilo!, ingawa mwanzo wake ulikuwa mgumu ila haukumkatiza tamaa kuhahakikisha anapata mwisho wa wenye matunda mengi.

Ndicho alichofanikiwa kuwa nacho, mwisho wa safari yake ulikuwa wenye mafanikio makubwa sana.

Mafanikio ambayo yaliondoa utawala wa Liverpool kwenye soka la England.

Vikombe 38 ndani ya miaka 27 ulikuwa ushindi mkubwa sana kwake.

Aliwazoesha mashabiki wa Manchester United furaha, kwao wao kushinda vikombe ilikuwa desturi yao.

Mzee Sir Alex Ferguson alijua jinsi ya kutengeneza timu ya ushindi. Hakuweza kusajili majina makubwa ila alikuwa anasajili vipaji vikubwa ambavyo aliishi navyo vizuri na kupata mafanikio.

Ndiyo maana dunia itamkumbuka kwa kutumia vipaji vya “class of 92” kutengeneza timu ambayo ilishinda vikombe vitatu (FA, EPL, UEFA CHAMPIONS LEAGUE) mwaka 1999.

Class of 92

Ilikuwa ngumu kuamini vijana wenye umri mdogo kutoka katika academy ya Manchester United wakimpa ushindi mkubwa Manchester United.

Kwa Sir. Alex Ferguson alijua namna ya kutumia wachezaji aliokuwa nao kupata mafaniko ndani ya timu.

Ndipo hapo mashabiki wa Manchester United walipokuwa walevi rasmi wa mafanikio.

Kwao wao timu kupata kikombe hasa hasa cha ligi kuu lilikuwa jambo ƙla lazima ndiyo maana walivunja rekodi ya Liverpool na kuwa timu iliyobeba vikombe vingi vya ligi kuu na timu yenye mafanikio makubwa ndani ya ardhi ya malikia.

Mashabiki wakawa wanaamini kuwa wao ni fahari ya nchi ya England. Alama na nembo ya nchi ya England walikuwa wameibeba wao wenyewe.

Waliamini wao ni watawala halisi wa nchi ya England ila walichokosea ni kusahau kuwa kila utawala huwa na nyakati zake.

Nyakati za Sir. Alex Ferguson ziliisha, na kwa bahati mbaya zilimalizikia na utawala wa Manchester United pale England.

Mapinduzi mengi yalifanyika, uwepo wa Chelsea ulionesha nuru kuwa itakuja kuwa timu ambayo itatingisha falme za Manvhester United.

Uwekezaji wa majerani zao (Manchester City), umekuja na shambulio la huzuni ndani ya timu ya Manchester United.

Pep Guardiola amechukua utawala wa jiji ƙla Manchester United, anakula kila anachojisikia, moyo wake ukitamani Pizza asubuhi mikono yake itatumwa iingie kwenye kinywa ili uufurahishe moyo.

Ana kila kitu kinachompa furaha na nguvu ya kuonekana yeye ni imara kwa sasa kuzidi Manchester United.

Kitu hiki kinawaumiza sana Manchester United, wenyewe wanaona walistahili kuwa na nguvu waliyonayo Manchester City kwa sasa.

Wanaamini neno mafanikio liliumbwa kwa ajili yao tu kanakwamba hakuna mtu mwingine anayetakiwa kupata mafanikio zaidi yao.

Hapa ndipo ugomvi wao na Jose Mourinho unapoanzia. Wakati anakuja Manchester United wengi waliamini ni kocha mwenye DNA ya vikombe.

Waliona dalili zote kupitia kwake kuwa watachukua ubingwa wa ligi kuu ya England kupitia Jose Mourinho.

Imekuwa tofauti na matarajio yao, Jose Mourinho haoneshi dalili ya kuwapa kikombe hicho kwa sababu wapinzani wake wako imara kuzidi yeye.

Mpira wake umekuwa hauvutii, matokeo ya uwanjani yamekuwa hayaridhishi kitu ambacho kinawafanya mashabiki wa Manchester United kutoandaa ƙleso ya kufutia machozi kipindi Jose Mourinho atakapoondoka kwa sababu ameshindwa kukifuta kivuli cha Sir. Alex Ferguson.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x