Hivi Messi alikuwa mzito kwenye miguu ya Singano?
Ramadhani Singano "Messi", ndivyo tulivyoamua kumbatiza hilo jina baada ya kuhadaika na mguu wake wa kushoto. Mguu ambao alikuwa akiutumia vizuri kukokota mipira na kupiga vyenga ambavyo viliwafanya mashabiki kutoa tabasamu. Tabasamu ambalo lilikuja na ubatizo mkubwa kwa Ramadhani Singano, jina lake lilionekana halifai tena kutumika, Messi akawa mtu sahihi...