EPL

Kwa leo Wembley utakuwa uwanja mgumu kwa Arsenal

Sambaza....

Kwa miaka ya hivi karibuni North London Derby imekuwa na mvuto kutokana na Tottenham Hotspurs kuwa timu ya ushindani tofauti na miaka mingi ya nyuma.

North London Derby ya 195 itakayopigwa katika uwanja wa Wembley, wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23. Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika uwanja wa Wenbley ilikuwa mwaka 1995 katika nusu fainali ya FA ambayo Arsenal alishinda goli 1 goli la Tony Adams.

Leo hii wanakutana katika mazingira tofauti na ya mwanzo. Mauricio Pochettino amefanikiwa kuitengeneza timu yenye ushindani hali ambayo inaonesha mechi hii itakuwa ya ushindani sana.

Kwanini nasema hivo??

Arsenal imekuwa na historia nzuri dhidi ya Tottenham Hotspurs, katika mashindano yote
Tottenham ameshinda mechi 56 dhidi ya Arsenal na kutoa sare michezo 49 wakati
Arsenal akishinda mechi 76.

Hii ni historia ambayo ilitengenezwa kipindi ambacho Arsenal ikiwa bora dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Msimu huu Tottenham Hotspurs imekuwa na matokeo ya kupanda na kushuka, lakini tangu afungwe na Manchester City katika uwanja wa Etihad mpaka sasa hajafungwa mechi yoyote katika michezo nane zilizopita, akiwa amefanikiwa kufunga magoli 20 na kupata clean sheets nne (4) katika michezo hiyo minane.

Inaonekana Tottenham Hotspurs imeshauzoea uwanja wa Wembley?

Mwanzoni mwa ligi Tottenham Hotspurs ilikuwa inahangaika kupata matokeo chanya katika uwanja wa Wembley na hii ilitokana na sababu mbili, ya kwanza ulikuwa uwanja mgeni kwao hivo kuna wakati walikuwa wanajiona ugenini muda mwingi.

Sababu ya pili vipimo vya Wembley ni vikubwa ukilinganisha na vipimo vya White Hart Lane

Kiufundi uwanja ambao unavipimo vidogo huwa unabana kipindi unapotengeneza mashambulizi, ukizoea kutumia uwanja wenye vipimo vidogo itakupa mtihani mgumu kwako wewe pindi unapoanza kutumia uwanja wenye vipimo vikubwa.

Mwanzoni hiki kitu kiliwapa wakati mgumu sana Tottenham Hotspurs, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda wanaonekana kuuzoea uwanja huu

Mpaka sasa Tottenham Hotspurs wamecheza michezo 12 katika uwanja wa Wembley bila kufungwa huku wakiwa wamefunga magoli 32 katika uwanja huo.

Hiki ndicho ƙkitu ambacho kinaonesha utayari wa Tottenham Hotspurs katika kutumia uwanja huu, na ugumu wa mechi hii unaanzia hapa kwa sababu Arsenal ameenda katika uwanja wa Wembley kwa miaka minne na kufanikiwa kubeba makombe matatu ya FA. Mara ya mwisho kwa Arsenal kufungwa kwenye uwanja wa Wembley ilikuwa mwaka 2011 kwenye fainali ya Carling cup dhidi ya Birmigham City.

Leo hii Arsenal inaenda Wembley ikiwa na rekodi mbovu msimu huu inapocheza ugenini, imetoka kufungwa mechi mbili za ugenini dhidi ya Afc Bournamouth na Swansea City.

Na mara ya mwisho kwao wao kushinda ugenini ilikuwa December 28 mwaka jana aliposhinda dhidi ya Crystal Palace.

Kipi kimekuwa kikiwagharimu Arsenal katika mechi za ugenini??

Hapana shaka safu yao ya ulinzi imekuwa ikifanya makosa mengi binafsi. Haina maelewano na hawajipangi vizuri hasa hasa wanapokuwa wanashambuliwa kwa mashambulizi ya kushitukiza “counter attacks”.

Mara nyingi wanapokuwa wanashambuliwa mabeki hufuata mtu aliye na mpira hali ambayo hutengeneza uwazi eneo la nyuma, uwazi ambao hushindwa kuzibwa kutokana na kukoseana kwa mtu wa kuziba ( ku cover), hivo hujikuta wanafungwa magoli mepesi.

Kwa aina ya wachezaji wa mbele wa Tottenham Hotspurs kwa kasi yao ni virahisi sana kuwalazimisha Arsenal kutengeneza uwazi katika eneo la nyuma.

Tottenham Hotspurs mechi kadhaa zilizopita ilikuwa na tatizo hilo lakini kurejea kwa Toby Alderweireld kutakuwa na msaada kwao kwa sababu siyo beki ambaye anaweza kutengeneza uwazi eneo la nyuma, lakini kama Arsenal wakilazimisha kuna uwezekano wa yeye kutengeneza uwazi katika eneo la nyuma.

Je ni kwa namna gani Arsenal wanatakiwa kumlazimisha Toby Alderweireld kutengeneza uwazi eneo la nyuma?

Tukumbuke atacheza eneo la beki wa kati upande wa kulia, upande ambao Trippier aracheza kama beki namba mbili.

Trippier amekuwa na kiwango kizuri hivi karibuni, amekuwa akitengeneza nafasi nyingi za kufunga kupitia krosi, namna pekee ya kuepukana na madhara haya kutoka kwa Trippier , Arsenal wanatakiwa wamfanye awe busy kukaba, kipindi mashambulizi yatakapozidi katika upande wake, lazima Toby Alderweireld aje upande wa kulia kumsaidia kukaba, anapokuwa anakuja upande huu basi atakuwa ameacha uwazi eneo la katikati hivo kutawapa nafasi nzuri kwa Arsenal kutumia uwazi huo.

Pili, Arsenal wanatakiwa wawalazimishe mabeki wa kati wa Tottenham Hotspurs kukabia eneo la mbele ili eneo la nyuma liwe wazi.

Uwepo wa Harry Kane utakuwa na madhara kwa Arsenal, tangia akutane na Arsenal kwa mara ya kwanza mwaka 2015 amefanikiwa kuifunga magoli 5. Na amekuwa na kiwango kizuri katika uwanja wa Wembley akiwa amefunga magoli 7 katika mechi 5 zilizopita katika uwanja huu.

Eneo lipi Spurs wanajivunia kwa sasa??

Eneo lao la kiungo ambalo limekuwa na watu wengi wanaoshuka katikati kuwasaidia Dier na Dembele. Son, Erricksen na Delle Alli wamekuwa wakishuka katikati kwa nyakati tofauti kuongeza idadi ya wachezaji katika eneo la katikati mwa uwanja.

Hii inaenda sambamba na kiwango cha Son katika uwanja wa Wembley ambaye kahusika katika magoli 8 kwenye michezo 6 aliyocheza Wembley, amekuwa na msaada mkubwa kwa spurs.

Pierre Emirick Aubameyang rekodi yake dhidi ya Tottenham hotspurs ina nafasi katika mechi ya leo?

Amefanikiwa kuwafunga spurs magoli manne katika mechi nne alizowahi kukutana nazo.

Hii inampa ujasiri mkubwa kuelekea mechi ya leo , ujasiri ambao utamwezesha yeye kufanya vizuri

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x