Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
EPL

Nini tatizo la Chelsea Msimu huu?

Msimu jana ulikuwa msimu wa kwanza kwa kocha Antonio Conte akiwa Chelsea. Pamoja na kwamba ulikuwa msimu wake wa kwanza akiwa kama kocha wa Chelsea, na msimu wa kwanza kwake akiwa kwenye nchi ya England lakini alifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya England. Antonio Conte aliikuta Chelsea ikiwa imefanya...
Ligi Kuu

CAF Yataja Waamuzi Wa Mechi Za Kimataifa Kwa Simba Na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF limetoa orodha ya waamuzi watakaotumika katika hatua ya awali ya michezo ya Ligi Ya Mabingwa Barani Africa na Kombe La Shirikisho itakayopingwa kuanzia mwezi ujao. Kwa Tanzania itawakilishwa na vilabu Kongwe hapa nchini, YangaFC kwenye Klabu Bingwa na SimbaSC kwenye Kombe La...
Ligi Kuu

Haukuwa muda sahihi kwa Pierre kuja Simba

Rasmi Simba jana imeingia mkataba na kocha Mfaransa Pierre Lenchantre na anatarajiwa kuanza kazi na kikosi cha Simba jumanne. Ni kocha mwenye elimu kubwa ya ukocha , hapana shaka ana mafanikio makubwa pia katika mpira wa Afrika. Mshindi wa Afcon mwaka 2000 akiwa na Cameroon na akafanikiwa kuwa kocha bora...
Ligi Kuu

Kocha mpya Simba aliwahi fukuzwa baada ya mechi tatu tu!

Leo klabu ya Simba imemtangaza Pierre Lechantre kuwa kocha mkuu wa Simba akisaidizana na Masoud Djuma ambaye alichukua ana kaimu nafasi iliyoachwa wazi na kocha Joseph Omong. Pierre Lenchantre ni kocha mwenye elimu kubwa ya ukocha akiwa na cheti cha UEFA pro licence, cheti cha ngazi ya juu kabisa ya...
Ligi Kuu

Kipi kifanyike ili Yanga ifanye vizuri Klabu Bingwa

Yanga ndiyo bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara. Usisahau kuwa ndiyo atakuwa mwakilishi wetu katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwezi ujao wa pili. Michuano ambayo ni migumu kwa sababu inakutanisha mabingwa wa Afrika. Hapa unatakiwa uwe na kikosi kipana na imara ili kuweza kushindana katika michuano hii,...
Ligi Kuu

Bernabeu Ilisimama, Leo Dunia imesimamishwa kichwa

Hakuna kitu kigumu kama kucheza katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Uwanja ambao wachezaji nguli washapita pale na kuweka rekodi nyingi za soka duniani. Uwanja ambao una mataji mengi ya kombe la klabu bingwa barani ulaya. Kombe ambalo lina ushindani mkubwa lakini wao ndiyo Wafalme kwa kulichukua. Wao ndiyo waliochukua mara...
Ligi Kuu

Kiyombo geuka nyuma umwangalie Bahanuzi

Hapana shaka umepata sifa nyingi, kila mtu anafurahia kutaja uwezo wako mahiri. Mwingine atasema unajua kutumia miguu yote miwili. Huyu akaja na jambo lake la wewe kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli ya mbali kwa mashuti makali. Tena huyu atamalizia kwa kusema anafunga magoli ya kiume. Ili mradi tu...
EPL

Maeneo yaliyomuwezesha Klop kumshinda Pep

Jana Jurgen Klopp alifanikiwa kuvunja utawala wa Manchester City wa kwenda mechi mechi 22 bila kufungwa. Anazidi kujiwekea rekodi nzuri dhidi ya Pep Guardiola, mpaka sasa katika michezo 12 waliyokutana Jurgen Klopp kafanikiwa kushinda michezo 6 na kutoka sare mchezo mmoja huku Pep Guardiola akishinda mechi 5. Jana Manchester City...
EPL

Liverpool ina nafasi kubwa kuifunga Man City

Leo kuna mechi ambayo inawakutanisha Liverpool na Manchester City katika uwanja wa Anfield. Mechi ya mzunguko wa kwanza Manchester City alifanikiwa kuifunga Liverpool goli 5-0. Leo hii wanakutana wakati ambao Liverpool anatafuta nafasi ya kubaki kwenye nafasi nne za juu na Manchester City akitafuta nafasi ya kujichimbia juu. Manchester City...
Uhamisho

Sehemu ipi sahihi kwa Sanchez? Manchester City au United?

Kuna habari za kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kuonekana kumtaka Alexis Sánchez, mchezaji kutoka kwa hasimu wake mkubwa, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal FC). Hii ni baada ya taarifa za awali kuonekana Manchester City kumwihitaji Alexie Sanchez tangu dirisha la usajili la majira ya joto na dirisha hili la...
1 75 76 77 78 79
Page 77 of 79