Mikono Ya Kabwili Inapingana Na Hukumu Yetu Kwake
Nilikuwa naangalia marudio ya mechi ya Saint Louis na Yanga iliyochezwa Usherisheri. Katikati ya mechi nilibaki naangalia umbo la golikipa wa Yanga, Youthe Rostand. Umbo ambalo linamfaa golikipa yoyote kuwa nalo. Kimo chake kizuri , kimo kinachompa sifa ya ziada kama golikipa. Kuwa na umbo zuri hakutoshi kukufanya kuwa golikipa...