Sambaza....

Meneja wa klabu wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ameshatakiwa na chama cha soka cha Uingereza (FA) kwa kosa la kuvaa riboni yenye ujumbe wa kisiasa

Meneja huyo alivaa riboni hiyo, kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic ambapo alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuondolewa kunako michuano hiyo

Taarifa zaidi zinasema kuwa Pep alivaa riboni yenye ujumbe huo, kwa kusudio la kuwasapoti wafungwa wa kisiasa wa Katalunya ambao wamefungwa gerezani nchini Hispania

Kwa mujibu wa chama hicho cha soka nchini Uingereza, sheria na taratibu za soka haziruhusu mpira kuhusishwa na masuala ya kisiasa, hivyo wameamua kumchukulia hatua meneja huyo

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni wanasiasa wa jimbo la Katalunya walikuwa wakipigania kujitenga kwa jimbo hilo na kutambuliwa kama nchi kamili

Sambaza....