Sambaza....

Ligi kuu ya soka Tanzania bara kuendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa kunako dimba la Samora mjini Iringa, amabo mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC watakuwa wageni wa Lipuli FC

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na rekodi za timu zote katika michezo ya hivi karibuni, ambapo Lipuli FC wameshinda mchezo mmoja kati ya 10, waliyocheza huku wakienda sare mechi 4, na kupoteza 5, huku Azam FC wakiwa hawajapata ushindi tangu walipofungwa na Simba sc Februari 7 na kuambulia sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Kagera sugar kunako dimba la Kaitaba mjini Bukoba

Katika mchezo huo Azam FC itawakosa nyota wake wanne, Salum Abubakar mwenye matatizo ya kifamilia Daniel Amoah aliyemajeruhi Waziri Junior anayetaraji kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu huku nahidha Himid Mao aliyekwenda Afrika kusini kwa matibabu ya goti, lakini habari njema kwao ni urejeo wa mlinzi Aggrey Morris aliyemaliza kutumikia adhabu ya kadi tatu za manjano

Huo ukiwa ni mchezo wa tatu kuzikutanisha timu hizo, kwenye mchezo wa kirafiki Azam FC walishinda kwa mabao 4-0 kabla ya kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi mzunguuko wa kwanza kunako uwanja wa Azam complex

Tayari kocha mkuu wa Azam FC Aristica Cioaba ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo

Sambaza....