kuibuka na kushindania ubingwa wa Ligi kama ambavyo aliwahi kufanya Leicester City katika EPL. Ni ngumu kutokea kwa maajabu kama haya, ni wazi sasa Simba ataendelea kutesa katika kutwaa ubingwa wa Bara.
Waswahili hutumia neno "Gundu" kwa kuashiria bahati mbaya, kukosa bahati ama mkosi, ndicho unachoweza kusema kwa timu zote mbili Simba na Yanga kuelekea mchezo wao wa nusu fainali wa Azam Sports Federation Cup.
Mara ya mwisho kwa Namungo FC kufungwa ilikuwa dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa walipofungwa magoli 3-2 . Tangu hapo wamepitia mechi 19 bila kufungwa na leo watakuwa wanatafuta mechi ya 20 bila kufungwa.
Endapo atapoteza mchezo tena dhidi ya Yanga huenda ikakoleza safari yake yakutimuliwa na Simba na kuache rekodi mbovu miongoni mwa makocha waliopita Simba mbele ya Yanga.