Blog

Shomari Kapombe kuivaa Yanga …

Sambaza....

Kwenye mechi ya nusu fainali kati ya Azam FC na Simba kulitokea tukio ambalo lilisababisha majeraha ya mchezaji wa Simba anayecheza nafasi ya beki wa kulia , Shomari Kapombe.

Shomari Kapombe alichezewa rafu mbaya na Frank Domayo ambaye ni kiungo wa Azam FC , rafu ambayo wengi waliona kama rafu ya makusudi na wengi walilalamika kwa kuonesha Frank Domayo hakufanya kitu cha uungwana.

Rafu hii ilimsababisha Shomari Kapombe kutolewa nje na kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na majeraha hayo yaliyotokana na rafu ya nahodha wa Azam FC , Frank Domayo.

Akizungumza na mtandao huu msemaji wa mkuu wa Simba , Haji Manara amedai kuwa Shomari Kapombe pamoja na beki wa kati , Kennedy Juma kwa sasa wanaendelea vizuri na hawakupata majeraha makubwa.

“Hawakupata majeraha makubwa kwa mujibu wa uchunguzi wa awali , ila jumatatu tunaweza kutoa taarifa zilizokamilika kuhusiana na majeraha yao. Lakini kwa sasa hakuna kitu kikubwa kilichowatokea”- alisema Haji Manara .

Kwa kauli hiyo inaonesha Shomari Kapombe anaweza kuwa mmoja ya wachezaji watakaocheza katika mechi ya nusu fainali ya Azam Federation Cup inayowakutanisha na watani wao wa jadi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.