Niyonzima
ASFC

Haruna Niyonzima kuikosa Simba.

Sambaza....

Kiungo Haruna Niyonzima huenda akaikosa mechi ya nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup ama kombe la FA baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Biashara United.

Niyonzima anaonekana ameumia goti baada ya kugongana na wachezaji wawili wa Biashara United dakika za mwanzo tu za mchezo wa Ligi uliomalizika kwa suluhu katika uwanja wa Karume Mara.

Haruna Niyonzima akipiga mpira mbele ya nahodha wa Simba Mohamed Hussein katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya ajali hiyo Niyonzima alishindwa kutembea na kutolewa nje kwa msaada wa wahudumu wa huduma ya kwanza huku akiangaliwa kwa umakini na jopo la utabibu la klabu ya Yanga.

Kama Yanga itamkosa Haruna katika mchezo dhidi ya Simba wa nusu fainali ya FA basi inazidi kupata pigo baada ya pia kutegemewa kumkosa Balama Mapinduzi na Mohamed Banka, huku pia nahodha Papy Kabamba akiwa ametoka kupona majeraha ya goti hivyo hakuna uhakika wa asilimia 100 kama atakuepo katika mchezo huo.

Tovuti yako pendwa ya Kandanda.co.tz itaendelea kufwatilia ni kwa kiasi gani Haruna amepata majeraha na atakaa nje kwa muda gani pindi ambapo ripoti ya kidaktari itakapotoka.

Sambaza....