Ligi Kuu

Kagere afunikwa na Chirwa

Sambaza....

Mzambia Obrey Chirwa ameandika
rekodi usiku  wa Julai 5 baada ya
kuwa mchezaji wa kwanza kwa
msimu huu kufunga hat trick mbili
katika Ligi Kuu Bara, wakati
akiiongoza Azam FC kuisambaratisha
Singida United iliyotangulia mapema
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutoka
Ligi Kuu.

Nyota huyo wa zamani wa Yanga na
FC Platnum ya Zimbabwe,
ameshafunga mabao manne mpaka
sasa wakati Azam ikiongoza kwa
mabao 7-0 katika pambano la upnde
mmoja linalopigwa Uwanja wa Azam
Complex.

Chirwa

Hat trick hiyo ni ya pili kwa Chirwa
baada ya ile ya kwanza dhidi ya
Alliance ya Mwanza walipoifumua
mabao 5-0 na kumfunika mpaka
Meddie Kagere wa Simba ambaye
licha ya makali yake tangu atue
nchini, hajawahi kufunga hat trick
mbili katika msimu mmoja.

Kagere naye alifunga mabao manne
walipovaana na Singida na
kuwafumua mabao 8-0, lakini
hajawahi kufunga mara mbili ndani
ya msimu mmoja, licha ya msimu
uliopita kumaliza kama kinara wa
Ufungaji akiwa na mabao 23.

Pia hii ni mara ya pili kwa Chirwa
ndani ya msimu mmoja kupiga hat
trick, kwani alifanya hivyo mra ya
kwanza msimu wa 2017-2018
alipozitungua timu za Mbeya City
wakati wakiishindilia mabao 5-0
katika mechi ya Novemba 19, 2017
kisha kurudia tena dhidi Njombe Mji
walioifumua 4-0 kwenye mchezo
uliopigwa Feb 06, 2018.

Meddie Kagere akipiga mkwaju wa penati katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Mabao hayo manne ya Chirwa
yamemfanya kufikisha mabao 12
akilingana na Reliants Lusajo wa
Namungo na kuzidi kukoleza vita ya
ufungaji bora inayoongozwa na
Kagere mwenye mabao 19 akifuatiwa
na Yusuf Mhilu wa Kagera Sugar
mwenye 13 akiwa nafsi ya pili.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.