Sven akiwa na timu yake ya ufundi
Ligi Kuu

Ngoma ngumu lakini sherehe lazima inoge!

Sambaza....

Kocha mkuu wa Simba Sven Bandebroek na nahodha wake John Raphael Bocco wameahidi ushinde kwa Wanasimba leo katika mchezo dhidi ya Namungo kwa mashabiki wao ili kunogesha sherehe za kukabidhiwa kombe lao. Kocha na nahodha wametoa ahadi hiyo walipokua wakiongea na tovuti ya klabu yao ya Simba.

Kuelekea mchezo wa leo kocha mkuu, Sven Vandenbroeck amesema anafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na uimara wa wapinzani lakini atahakikisha tunapata ushindi ili kunogesha sherehe za kukabidhiwa taji letu la ubingwa.

Sven “Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu, Namungo ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri lakini kwakua tunaenda kukabidhiwa ubingwa, tutahitaji kupata ushindi.”

John Raphael Bocco “Adebayor”

Kauli ya kocha Sven inaungwa mkono na nahodha John Bocco ambaye amesema mchezo utakuwa mgumu lakini kama wachezaji wamejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili kutotia doa sherehe za ubingwa.

“Tunaiheshimu Namungo ni timu nzuri na ipo kwenye kiwango bora kwa sasa na tunaenda kucheza kwenye uwanja wao tunajua mechi itakuwa ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” Nahodha John Bocco.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.