Shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha kuwa michezo miwili ya nyumbani ya African Lyon dhidi ya Simba na Yanga itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini Arusha.
Habari ambazo zimeenea na viongozi wa Yanga kuwa na kigugumizi kuthibitisha ni kuwa kiungo wa African Lyon na aliyewahi kuchezea Simba, Haruna Moshi "Boban" kuwa amesajiliwa na klabu ya Yanga.