Ligi KuuUhamisho

BOBAN atakuwa na faida kubwa kwa Yanga!

Sambaza....

Habari ambazo zimeenea na viongozi wa Yanga kuwa na kigugumizi kuthibitisha ni kuwa kiungo wa African Lyon na aliyewahi kuchezea Simba, Haruna Moshi “Boban” kuwa amesajiliwa na klabu ya Yanga.

Kama itakuwa ni kweli basi yafuatayo ni maeneo ambayo Haruna Moshi “Boban” atakuwa na msaada ndani ya kikosi cha Yanga.

Haruna Moshi Boban anaweza akawa na msaada mkubwa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo?

Kwa hali ya Yanga ilivyo (kiuchumi) inahitaji watu wengi ambao wanaweza kuwajenga wachezaji wapigane katika ugumu wa mazingira wanayoyapitia kiuchumi.

Inawezekana Haruna Moshi “Boban” akawa hana msaada mkubwa sana ndani ya uwanja lakini akawa na msaada mkubwa sana kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Haruna Moshi Boban (Akihojiwa na Azam TV)

Kwa hiyo ujio wa Haruna Moshi “Boban” utakuwa na msaada mkubwa sana katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Yanga, kuna uwezekano mkubwa Haruna Moshi “Boban” akawa ameleta asilimia kadhaa ya morali ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Haruna Moshi “Boban” atakuwa ameongeza idadi ya viongozi ndani ya uwanja?

 Amekuwa nahodha wa African Lyon kwa msimu huu, hii inaonesha ana chembe chembe za kuwa kiongozi ndani ya timu. Tangu Nadir Haroub aondoke, Yanga hawajawahi kuziba pengo la uongozi la Nadir Haroub. Kuna umuhimu sana timu kuwa na wachezaji wengi ambao wana sifa ya kiungozi.

Nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub, sasa ni Meneja wa Timu.

Kwa timu ya Yanga ina uhaba wa aina hii ya wachezaji, kwa kutazama Kamusoko na Yondani ndiyo pekee ambao wana sifa ya kuwa viongozi ndani ya timu.

Kwa hiyo kuja kwa Haruna Moshi “Boban” kutaongeza idadi ya wachezaji viongozi ndani ya timu. Pia kuja Haruna Moshi “Boban” kutaifanya Yanga iwe imeziba pengo la Nadir Haroub ndani ya uwanja kama kiongozi.

Uzoefu wake una nafasi gani kwenye timu ?

Amedumu kwenye mpira wetu kwa muda mrefu, anajua soka letu. Hivo hii itakuwa na msaada mkubwa kwa Yanga kutumia uzoefu wake kuisaidia timu hasa hasa kipindi hiki ambacho inahitaji ubingwa wa ligi kuu.

Anaweza kuwa mbadala sahihi wa Ibrahim Ajib?

Siyo rahisi kihivo, lakini anaweza kuisaidia Yanga kipindi ambacho Ibrahim Ajib amepata majeraha ingawa hatokuwa na msaada mkubwa kama anavyofanya Ajib.

Ajib

Kuna wakati Ajib akikosekana timu huwa inatumia nguvu nyingi sana kutengeneza nafasi za kufunga. Haruna Moshi “Boban” ni mzuri katika kutengeneza nafasi za kufunga.

Je ataingia kwenye mfumo upi mzuri ?

Ili kumwingiza kwenye moja kwa moja , Yanga watatakiwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1. Ambapo katikati watakaa viungo wawili (Fei Toto pamoja na Kamusoko au Tshishimbi). Na mbele yao watakaa watu watatu ambao ni Ajib , Boban na Ngassa huku mbele akibaki kusimama Makambo.

Haruna Moshi “Boban” atakuwa na msaada mkubwa ndani ya msimu huu tu, na Yanga kwa kipindi hiki kigumu wanatakiwa kuwa na aina ya wachezaji ambao wanaweza kutembea kwenye kipindi kigumu ili kuisaidia timu.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x