Sambaza....

Baada ya kitecho alichofanya mlinzi wa Yanga sc, Kelvin Patrick Yondan, kumtemea mate Asante Kwasi katika mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara dhidi ya Simba, Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa tamko

Afsa habari wa Shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo, amesema kuwa bado hawajapokea malalamiko kutoka klabu ya Simba kuhusiana na suala hilo

Mbali na malalamiko kutoka Simba, Ndimbo ameweka wazi kuwa wao hutegemea ripoti ya Kamisaa wa mchezo ili kufanya tathimini na kubaini wapi kulikuwa na mapungufu ili kufanyia kazi

Akifafanua zaidi, Ndimbo alisema kuwa endapo Simba wakifikisha malalamiko yao ndipo taratibu zingine zitafata lakini kwa sasa lakini kwa sasa hawawezi kufanya chochote

Katika mchezo huo, ambao Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 kamera zilimuonesha Yondani akimtemea mate Kwasi ikiwa ni kipindi cha kwanza cha mchezo huo, lakini mwamuzi hakuliona tukio hilo

Sambaza....