Ligi Kuu

Simba yaangukia pua mbele ya Wanajeshi

Sambaza....

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti wameshindwa kuanza vyema katika mchezo wao wakwanza wakufungua ligi hiyo baada ya kupoteza mchezo katika uwanja wao wa nyumbani.

Ligi ya Wanawake imeanza rasmi leo ambapo JKT Queens walikua wageni wa Simba Queens katika uwanja wa MO Arena na kushuhudia Simba Queens wakipoteza mchezo kwa mabai mawili kwa moja.

Simba ndio waliokua wakwanza kupata bao kupitia kwa kwa mkwaju wa penati uliopigwa na mshambuliaji wao hatari Opa Clement “Drogba” katika dakika ya 24.

JKT walitulia na kusawazisha goli la kwanza katika dakika ya 32 na kupata bao la ushindi dakika ya 45+1 kabla ya kwenda mapumziko. 

Simba ni kama hawakua na bahati katika mchezo huo licha ya kupoteza nafasi nyingi za wazi kupitia wa washambuliaji wake lakini pia walikosa penati iliyopigwa na Vivian Corazzone katika dakika ya 79. 

Mpaka mchezo unamaliza JKT Queens mbili na Simba 1 na hivyo mabingwa watetezi wa Ligi hiyo kuanza vibaya tena katika uwanja wao wa nyumbani. 

Sambaza....