Ligi Kuu

Abdalah Shaibu “NINJA” Ruksa kuivaa SIMBA

Sambaza....

Beki wa Yanga , Abdalah Shaibu “Ninja” atakuwa huru kucheza dhidi ya Simba katika mechi ya kesho baada ya kamati ya nidhamu ya TFF kukubali kusikiliza shauri lake.

Kukubali kusikilizwa kwa Abdalah Shaibu “Ninja” kutakuwa na maana ya kwamba adhabu yake imeondolewa mpaka pale kamati ya nidhamu ya TFF itakapomsikiliza.

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia ombi la Yanga la kuahirisha kusikiliza shauri dhidi ya Abdallah Shaibu kwa vile wakati anapata mwito wa kuhudhuria akiwa mkoani. Sasa shauri dhidi yake litasikilizwa katika kikao kijacho, na Kamati haitapokea udhuru wowote isipokuwa kama atakuwa na majukumu katika timu ya Taifa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.