Larry Bwalya
Blog

Makosa ya usajili wa Simba Sc. (02)

Sambaza....

Kama ilivyo kwa falsafa ya klabu ya Simba yaani kushambulia kwa kulitawala eneo la kati, hivyo inatubidi tukitazame kikosi cha Simba katika jicho hilo…

Tukianza na mstari wa mabeki, msimu huu Simba imewaongeza  Beki wawili wa kati, Joash Onyango na Ibrahim Ame ambao wote kiufundi ni wazuri zaidi katika nafasi ya kati upande wa kushoto na wakiwa na maumbo tofauti.

Onyango ni mwenye mwili na nguvu, huku kimo chake kikiwa ni cha wastani, Ame ni mwembamba, Mrefu na mwenye nguvu pia.

Mabeki hawa wanaungana na Paschal Wawa, Kennedy Wilson na Erasto Nyoni, jumla Simba inakuwa na mabeki watano wenye uwezo wa kucheza kama mabeki wa kati.

Sifa yao kubwa ni maumbo makubwa na vimo virefu. Simba itaenda kuwa na mabeki warefu katikati, na wenye miili mikubwa. Sifa za maumbo yao ni wazuri katika uokoaji wa mipira ya kona kwa kupiga vichwa lakini pia kufunga.

Udhaifu wao mkubwa ni kasi… yaani wote ni wazito, lakini pia kati ya hao wote ni Paschal wawa pekee ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kucheza kama beki wa kati upande wa kulia, Onyango naye anacheza lakini anatumia uzoefu zaidi kuliko akiwa eneo la kushoto… hii ina maanisha kuwa, wengine wote watabadilishana upande wa kushoto kuliko kulia… hii ni hatari zaidi pindi Wawaanapokosekana.

Ukiachana na mabeki wa kati, Simba imemsajili David Kameta kutoka Lipuli kama beki wa kulia. Kameta ni mfupi, mwenye umbo la kawaida, mzuri wa kupiga mipira mirefu na ku-overlap. Kameta ni Rasmi sasa anaungana na Shomari Kapombe, Mohamedi Hussein na Gadiel Michael. Kiujumla wote ni wafupi, wote wanajua kumiliki mpira na kushambulia pembeni mwa uwanja,huku Kapombe akitofautiana na wenzie, yeye Kajazia zaidi yaani ana nyama.


Soma zaidi


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.