Ligi Kuu

Ali Kamwe: Mabeki wa Namungo waliizawadia Yanga ushindi.

Sambaza....

Mambo 10 nilioyaona YANGA vs NAMUNGO 

1: CLASSIC MATCH✊ 3 za KIBABE. 3 za KIKUBWA. 3 ZA KIBINGWA. Inahitaji akili ngumu, Nafsi Jasiri na moyo unaoweza kuishi motoni ukitabasamu ndio uamini kuna BINGWA MWINGINE WA LIGI TOFAUTI NA YANGA

2: Nilipenda jinsi makocha walivyoamua kushindana kimbinu. Kila ‘Sub’ ilikuja uwanjani na swali jipya kwa mpinzani.. Kaze ameshinda yake kwa Faida ya QUALITY PLAYERS kwenye kikosi chake.

Fiston Kalala Mayele


3: Namungo ni kama walijiandaa na Mechi 2. Dhidi ya YANGA na Dhidi ya MAYELE. Bahati mbaya zote wamepoteza. Bahati nzuri kwao wamepoteza bila kadi nyekundu kwenye kikosi chao.

4: Ukiwa na pacha ya BAKARI na BANGALA pale nyuma.. Aucho mbele yao.. Naamini kila kocha angetamani kufanya ‘Build Up’ kutokea chini.. Bado naendelea kutafakari Molinga huwa ana kitu gani cha tofauti katika uwanja wa mazoezi kiasi cha kumshawishi mwalimu kumpa dakika kuupress ‘Utatu’ wa Yanga kutokea nyuma.

Yanick Bangala.

5: Utatu wa Yanga chini. Mbele yao kuna ‘double Play Maker’ .. Feisal na Sure Boy🙌 Nilielewa kwanini Fredy Tangalo aliondolewa mapema uwanjani. Hii haikuwa mechi ya nguvu.. Ilikuwa mechi ya akili kubwa.

6: SURE BOY ANAENYOY GAME YAKE AKIWA NA JEZI YA YANGA🙌 WHAT A PLAYER. Ni ngumu kumuelezea Lakini ni rahisi kumuelewa.. DECO WA JANGWANI✊

7: SHIZA KICHUYA.. Hii ilikuwa zaidi ya mechi kwake. Alikimbia kilomita nyingi uwanjani kutafuta kilio kwa Yanga.. Nafikiri kama angekuwa na Chirwa/Lusajo mapema kiwanjani, Angekuwa na uhuru zaidi wa kusababisha madhara.

Lucas Kikoti akimuacha chini Salum Aboubacar wa Yanga.

8: Frank Magingi anaweza kumshukuru mwamuzi kwa wakati wake. Kadi nyekundu aliitafuta na alikaribia kuipata.. pale kwa AGGREY MORRIS Mayele alishathibitisha ili umzuie inahitaji AKILI, NGUVU NA UMAKINI MUDA WOTE

9: Kwa kiasi fulani ukuta wa Namungo ni kama ulitoa zawadi kwa mastraika wa Yanga. Mabao yote mawili.. UMAKINI. UMAKINI. UMAKINI.. bila shaka ndio wimbo utakaoimbwa na kocha kwenye uwanja wa mazoezi kesho.

Jesus Moloko (12) akimtoka mlinzi wa Namungo Erick Manyama (50).

10: MOLOKO amejidhulumu kuondoka bila bao. Lucas Kikoti ni Fundi asiyehitaji utambulisho.. Nilipenda sana nidhamu/Perfomance ya MAKAME uwanjani.

Ali Kamwe.

Sambaza....