Sambaza....

Kocha msaidizi wa Timu ya soka ya Alliance Kessy Mziray ameimwagia sifa timu ya soka ya Mbao ambayo ilicheza vizuri katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi ya juma hili.

Mziray amesema Mbao ilikuwa bora zaidi hasa katika eneo la kiungo na ndio maana wao waliwazidi Mbao katika dakika 30 tu za mwanzo za mchezo huo lakini dakika zote hata pale Mbao walipopata kadi nyekundu lakini bado walikuwa bora kuwazidi.

“Katika mchezo huu Mbao wametuzidi kwenye eneo la kiungo, walikuwa bora zaidi na ndio maana walituzidi sana kwenye mchezo wa leo, niwape sifa kwa kuwa walikuwa bora kimbinu, pengine kama wangekuwa makini matokeo yasingekuwa kama haya,” amesema.

Aidha Mziray amesema matokeo ya sare ya 0-0 ambayo wameyapata ni mazuri na yalikuwa katika mipango yao kwamba angalau wapate alama moja ili kujisogeza kutoka mkiani walipokuwa, amesema matokeo hayo yanazidi kuwaonesha kwa namna gani wamezidi kuimarika na hasa baada ya kufanya usajili.

“Matokeo ya sare yanatufanya kufikisha alama 21 sio mbaya, yamezidi kutosogeza kutoka pale tulipokuwa mwanzoni mwa ligi, pia ukiangalia mzunguko wa kwanza tulianza kwa kupoteza lakini sasa tumetoka sare hii inaonesha tunazidi kuimarika siku hadi siku, sasa tunaelekea Dar kucheza na African Lyon naamini matokeo yataendelea kuwa mazuri,” amesema.

Sambaza....