Ligi Kuu

Azam FC hawajui cha kufanya mbele ya pesa zao

Sambaza....

Ushawahi kuingia kwenye website ya Azam FC (tovuti ya Azam FC ?). Kuna maneno matamu utakutana nayo, maneno ambayo yatakufanya utoe tabasamu pana kabla ya kuendelea chochote. Tovuti ya Azam FC kwenye maneno ya mwanzo wanatuambia kuwa Azam FC imekuwa alama ya vilabu vya kisasa hapa Tanzania.

Maneno haya ukiyachukulia kama yalivyo lazima utatoa tabasamu pana. Wakati naendelea kusoma maneno haya ya mwanzoni niliwaza ipi vision na mission ya Azam FC?. Wamekuwa klabu ambayo ni nembo kama klabu ya kisasa Tanzania kama wanavyojitambulisha kwenye tovuti yao ila ipi ni vision yao ?

Swali hili lilinipa nguvu ya kusogea chini, kwa bahati nzuri nilikutana na vision ya Azam FC ambayo imeandikwa kwa kifupi sana na kwa kueleweka ndani ya Website yao. Vision yao (maono yao) ni kuhakikisha Azam FC inakuwa timu kubwa inayoongoza kwa mafanikio ndani na nje ya uwanja. Hapa ndipo nilipotulia kidogo nikasindikiza nilichosoma na fundo la maji.

Wakati hata sijatafakari kwa upana kuna swali jingine lilikuja katika akili yangu, ipi ni mission ya Azam FC? Yani wataifikia Vision (maono) yao kwa njia ipi ?

Wapo wanaoamini Azam FC ni suluhisho la maendeleo ya soka letu … lakini mimi sio mmoja wao

Wakati nashusha glass ya maji ya kunywa , niliamua kupeleka kidole changu cha mkono wa kushoto kwenye website yao tena. Nilishuka chini ambapo nilikutana na mission ya klabu.

Nilikohoa kidogo kama kujiandaa na kusoma kitu ambacho nilichokuwa na kitamani kukijua. Azam FC wanatuambia kuwa jinsi ya kufikia kuwa klabu kubwa na yenye mafanikio makubwa Tanzania wana njia moja tu.

Njia yao ni kuanzisha programu endelevu za maendeleo ya soka nje na ndani ya uwanja ili kuifanya klabu iwe yenye mafanikio ndani na nje ya uwanja.

Hapa ndipo nilipoamua kurudi nyuma kuanzia kwenye utambulisho wa klabu, utambulisho ambao ulikuwa unaonesha Azam FC ni alama ya klabu ya kisasa hapa Tanzania.

Nikawaza klabu ya kisasa ya mpira wa miguu ikoje ?, nilisita kidogo kuipa nafasi yangu kuwaza zaidi. Niliamua kuchukua simu yangu kwa ajili ya kumpigia mtaalamu wa utawala katika mpira wa miguu.

Huyu ni mkufu wa chuo cha michezo cha Malya pale Mwanza. Alipopokea simu yangu nilimuuliza swali moja tu, klabu ya kisasa ya mpira wa miguu inatakiwa kuwaje ?

Alikohoa kidogo, kisha akasindikiza kikohozi chake kwa kicheko. Kisha akaanza kwa kuniambia “Kiyumbi rafiki yangu hata salamu ni kitu cha muhimu sana duniani”.

Nilitulia baada ya kugundua nimefanya kosa. Nilimsalimia kisha akaenda moja kwa moja kwenye jibu la swali langu.

Aliniambia kuwa klabu ya kisasa ndani ya uwanja tu inatakiwa kuwa na watu zaidi ya 25. Nilikohoa kidogo na kuendelea kupata shauku ya kumsikiliza zaidi. Aliniambia timu inatakiwa kuwa na meneja, meneja msaidizi, kocha mkuu, kocha wa timu ya kwanza, kocha wa magolikipa,Physiologist, Doctors, Kit Manager (mtunza Vifaa).Assistant Kit Manager (mtunza vifaa msaidizi), First Team Strength and Conditioning Coach,Assistant Fitness Coach.Masseur,Nutritionist,First Team Physiotherapist,  Match Analyst,Soft Tissue Therapist.Dressers & Designer ,Life Style Consultancy,Data & Records Officer, Video/Photographer , Security Officers, Advance Part Teams, Hospitality and Accommodatio, Propaganda and protocol officer.

Kabla hata hajamaliza ni umbo gani la kiungozi ambalo klabu ya kisasa inatakiwa kuwa nalo. Nilimwambia Asante, kisha nikakata simu, nikarudi tena kwenye tovuti ya Azam FC.

Utambulisho wa klabu unaelezea kuwa Azam FC imekuwa nembo ya klabu ya kisasa hapa Tanzania !. Nikatulia na kuitazama Azam FC na kitu ambacho niliambiwa na mkufunzi wa chuo cha michezo cha Malya.

Azam FC wakishangiilia ushindi wao.

Niligundua kuna uwazi mkubwa kati ya vitu ambavyo niliambiwa na mkufunzi yule na uhalisia ambao upo kwenye timu ya Azam FC.

Kwenye vitu ambavyo niliambiwa na yule mkufunzi ni vichache sana ambavyo Azam FC wanavyo. Hapo ndipo nilianza kukuna kichwa kuhusiana na utambulisho wa Azam FC kwenye tovuti yao.

Kwa haraka haraka Azam FC ina kocha mkuu, kocha msaidizi, meneja wa timu, mratibu wa timu, daktari wa timu, mabaunsa, washangaliaji. Ukitazama hapa na alichokisema mkufunzi wa chuo cha Malya utagundua kuna uwazi mkubwa sana.

Kwa kifupi hakuna uhalisia wowote unaozungumzwa kwenye utambulisho wa website yao kuwa wao ni klabu ya kisasa.

Kuna vitu vingi hawana kuanzia kwenye timu, vitu ambavyo vinatakiwa kukamilisha ukisasa wa timu husika.

Kuna kitu kimoja ambacho huwa nakitazama kwa Azam FC. Kuhusu aina ya usajili ambao huwa wanafanya. Kuna swali moja ambalo huwa linazunguka sana kichwani mwangu.

Wale wachezaji ambao huwa wanasajiliwa kutoka nje ya nchi huwa kuna ma-scout maalumu wa Azam FC ambao huwa wanawafuatilia kwanza kabla ya kuwasajili?

Jibu ni hapana , hakuna Ma scout wa Azam FC ambao huhusika katika usajili wa wachezaji mbalimbali. Hapa ukisasa wa klabu unapungua na hakuna tofauti kabisa kati ya Simba , Yanga na Azam FC.

Ukitazama kwenye mission yao wanaonesha lengo lao la kutoa mafunzo mbalimbali ambayo yatakuwa na faida kubwa ya kimaendeleo katika klabu husika.

Kitu ambacho ni kizuri sana , na Azam FC wanakifanya ingawa siyo kwa asilimia kubwa. Ila Azam FC wanakifanya. Mfano wanatimu za vijana katika ngazi mbalimbali za umri.

Wanatimu za vijana za chini ya umri wa miaka 10, chini ya umri wa miaka 15, chini ya umri wa miaka 20, chini ya umri wa miaka 23. Kitu ambacho ni kizuri na wanatakiwa kupongezwa kwa kiasi kikubwa.

Azam FC wakiwa na kombe la Mapinduzi

Lakini kuna swali kubwa ambalo huwa linanisumbua sana. Hawa vijana kutoka kwenye hizi timu za vijana huwa wanaenda wapi ? , kuna utaratibu gani wa kuwaendeleza hawa vijana kutoka timu za vijana mpaka timu ya wakubwa?

Hawa si ndiyo huandaliwa kwa ajili ya kuwarithi kina John Bocco, Kipre Tcheche? Lakini kwanini huwa wanakimbilia kusajili wachezaji wa nje ambao hawana viwango vikubwa sana ?

Hakuna anayewalaumu kusajili nje lakini aina gani ya wachezaji ambao unawasajili na kuwaleta ndani ya timu ? , wanakiwango kikubwa kuzidi wa ndani au kiwango cha kawaida?

Asilimia kubwa ya wachezaji wa kigeni wa Azam FC hawana kiwango kikubwa cha kuisaidia Azam F kushindana kikamilifu.

Ndiyo maana ndani ya miaka 9 tangu wapande ligi kuu wamefanikiwa kushinda kombe la ligi kuu ya Tanzania bara Mara moja tu.

Huu ni ukweli uliowazi kuwa njia waliyotumia kipindi cha nyuma haijawafikisha kwenye mafanikio. Wanachotakiwa ni kutumia kituo chao cha vijana kwa ajili ya kupata mafanikio .

Tumewaona As Vita, Al Ahly ambao wana asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani katika kikosi chao. Azam FC wanatakiwa kutumia kituo chao kuzalisha wachezaji wa ndani ambao watakuwa na msaada kwenye timu yao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.