Kikosi cha JKT Tanzania kilichopanda daraja
Stori

Bado Moja JKT Tanzania Wapishane na Ruvu Shooting

Sambaza....

Ligi ya Championship zamani Ligi daraja la kwanza inakaribia kufika ukingoni huku timu zikiwa zimebakiza michezo minne ili kumaliza michezo yao yote. Wakati kwa upande wa Ligi Kuu mpaka sasa timu zote zimeshuka dimbani mara 26 wakibakiza michezo minne pekee.

Katika msimamo wa Championship kinara ni JKT Tanzania wakiwa na alama zao 56 katika michezo 25 waliyoshuka dimbani wakifwatiwa na Pamba wenye alama 51 na Kitayosce wote wakiwa na alama 50 katika nafasi za pili na tatu.

Kwa upande wa Ruvu Shooting wao wapo dhoofu na hali yao katika msimamo wa Ligi Kuu wakishika nafasi ya 15 yaani nafasi ya moja juu kutoka mkiani na alama zao 20 wakimuacha alama moja pekee Polisi Tanzania anayeburuza mkia.

Wachezaji wa Ruvu Shooting wakipasha misuli katika moja ya michezo ya Ligi Kuu

Maafande hawa ni kama sasa wanaelekea kupishana katika ligi hizi kwani JKT wanahitaji ushindi katika mchezo mmojaa pekee ili waweze kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka misimu miwili iliyopita. Wakati Ruvu Shooting wao wanahitaji ushindi katika michezo yao minne iliyobaki walau kufufua matumani ya kuchez hata Playoffs huku wakiwaombea mabawa wapinzani wap wengine waliopo nafasi za chini.

Kama JKT Tanzania watapa ushindi katika mchezo unaofuata April 22 ugenini dhidi ya Kitayosce basi watakua rasmi wamerudi Ligi Kuu baada ya kushuka msimu wa 2020/2021 wakiwa wanatumia uwanja wa Jamuhuri Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani.

Ruvu Shooting ni kama sasa wanakwenda kutoa nafasi kwa wenzao JKT Tanzania kwani kwa alama zao 20 wanahitaji kushinda michezo minne ili wafikishe alama 32 zilizo salama huku wakiombea Coastal Union, KMC, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons wapate matokeo mabaya katika michezo yao iliyobaki. Miongoni mwa michezo iliyobaki dhidi ya Azam nyumbani na Simba ugenini, kwa hali ilivyo ni vigumu kwa Maafande hao kutoboa na kupata alama zote 12.

Mshambuliaji wa JKT Tanzania Edward Songo akimuacha mlinzi wa Pan Africa.

Kama ikitokea hivyo ni dhahiri shahiri JKT Tanzania watakua wamerudisha burudani kwa wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kwani haswa wa maeneo ya Tegeta, Bokko, Mbweni, Bunju na Kunduchi kwani ndio timu pekee yenye uwanja Wilaya ya Kinondoni.

Wakati kwa upande wa wakazi wa Pwani kwao itakua ni kilio cha kukosa michezo ya Ligi kuu kwani ndio timu pekee mkoani humo inayoshiriki Ligi Kuu

Sambaza....