Uhamisho

Bakari Mwamunyeto, beki ghali Tanzania

Sambaza....

Jana Yanga imekamirisha usajili ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu wa beki kisiki wa Coastal Union na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Bakari Nondo Mwamunyeto.

Beki huyo ambaye alikuwa anawaniwa pia na mahasimu wakubwa wa Yanga ambao ni Simba. Yanga imewazidi Simba kwenye mbio hizi na kuhakikisha kuwa wamempata beki huyo.

Kwa habari za ndani zinadai kuwa Bakari Mwamunyeto amesajiliwa kwa dau la milioni 250 . Dau ambalo ni kubwa sana kuwahi kutokea kwa mchezaji mzawa .

Kwa dau hili linamfanya Bakari Nyundo Mwamunyeto kuwa beki ghali kwenye ligi kuu Tanzania bara. Pia amekuwa mchezaji ghali mzawa anayecheza ligi kuu Tanzania bara.

Luis Miqisoune wa Simba ndiye mchezaji ambaye amewahi kusajiliwa kwa dau kubwa kwenye historia ya ligi yetu , Simba walitoa dola laki moja kwa ajili ya usajili wake.

Kwa hiyo Bakari Nyundo Mwamunyeto anabaki kuwa mchezaji wa pili ghali kwenye ligi yetu baada ya Luis wa Simba ambaye ndiye anasimama kama mchezaji kinara ghali kwenye ligi yetu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.