Ally Ramadhani "Oviedo" akiwa mazoezini katika uwanja wa Bora Kijitonyama.
Blog

Beki KMC! Kama sio soka ningekua mwanajeshi!

Sambaza....

Tovuti ya Kandanda imepata nafasi ya kukutana na kupiga “story” mbili tatu na mlinzi wa kushoto wa KMC “Kino Boys”  Ally Ramadhani “Oviedo akiwa mtaani kwake na kufunguka mengi ambayo hukuwahi kuyasikia kutoka kwake.

Tovuti yako pendwa itakuletea mtiririko wa mambo mengi ambayo Oviedo ameiambia tovuti hii, Oviedo ni miongoni mwa wachezaji waliokaa na timu ya KMC tangu ipo Ligi daraja la kwanza mpaka ikapanda Ligi Kuu.

Oviedo ambae anaamini kama sio mpira wa miguu basi leo hii angekua anavaa gwanda na kutumikia jeshi kama ambavyo ndoto zake zivyokua tangu utotoni.

Ally Ramadhani “Oviedo”.

Ally Ramadhani “Kama isingekua kujihusisha na mpira ningekua Mwanajeshi, nilikua natamani sana kua vile. Lakini nashukuru Mungu kipaji cha mpira pia kimenifanya kufika hapa.”

Oviedo pia anaamini michuano ya mtaani “Ndondo” yanasaidia sana haswa kwa wachezaji wa Kitanzania kutokana na kuweza kuwapatia nafasi ya kuonekana na kujitambulisha katika soka. Ingawa sio rasmi.    Akisema kua kuna baadhi ya wachezaji wamefika au wameweza kucheza Ligi Kuu kutokana na kuonekana katika michuano hiyo.

Ally Ramadhani “Oviedo” akimpiga chenga kiungo wa Coastal Union Mtenje Albano!

“Michezo hiyo inasaidia kwa kiasi fulani, kwa maana kuna wachezaji wanaocheza Ligi mpaka leo kutokana na kuonekana katika michuano hiyo. Hivyo nafikiri sio kitu cha kukibeza kwa nchi yetu.

Ipo mifano mingi tuu, ambapo wachezaji mahiri tuu lakini walianzia katika ndondo mpaka leo wamekua muhimu katika vilabu vyao.” Ally Ramadhani ambae ameongeza kua mpaka sasa hakuna mechi ngumu au mchezo mgumu ambao amekutana nao tangu aanze kucheza soka kutokana na wachezaji wote ni walewale tuu ambayo wanakutana kila siku.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.