Ligi Kuu

Beki KMC: Nitafunga sana endeleeni kuhesabu tuu

Sambaza....

Kiraka wa KMC Sadala Lipangile mwenye uwezo wa kucheza nafasi mbili za ulinzi na ushambuliaji kwa ufasaha kabisa amesema ataendelea sana kufunga mabao katika VPL.

Sadala Lipangile aliibuka Galacha wa mabao kwa mwezi January na leo amefanikiwa kukabidhiwa  zawadi zake za kisheherekea na tovuti ya Kandanda ikishirikiana na Mgahawa Cafe and Restaurant katika uwanja wao wa mazoezi Bora Kijitonyama.

Kiatu cha Sadala

Baada ya kukabidhiwa mvinyo pamoja na kiatu chake alisema amefurahi sana kwa tovuti kutambua mchango wake katika ufungaji huku akiushukuru  Mgahawa Cafe&Restaurant kwa kumpa nafasi ya kupata chakula cha mchana katika mgahawa huo.

Sadalla Lipangile ” Nimefarahi sana kwa hizi zawadi ni kitu kikubwa sana kwangu, nimepata kumbukumbu sahihi kwangu na kwa timu. Inshaalah nategemea kuendelea kufanya vizuri ili niweze kuisaidia timu.

Sadala pia amesema anataka kufunga magoli zaidi na zaidi huku akiahidi kuongeza jitihada.

Sadalla “Mipango yangu ni kufunga magoli mengi japo siwezi kutaja idadi ya magoli lakini  naweza sema nitajitahidi kuongeza zaidi ya hapa. Naamini mtakuja tena kunikabidhi kiatu baada ya kuibuka tena Galacha wa mabao.”

Sadala pia hakusita kutoa shukrani kwa tovuti na mdhamini pia wa tuzo hiyo Mgahawa Cafe&Restaurant.

Sadalla Lipangile ” Nawashukuru sanasanaa kwa hiki mlichonipa hakika mmeonyesha kuona na kuthamini hiki nilichokifanya. Nafurahia hiki kiatu lakini pia ni furaha kupata nafasi ya “lunch”  Mgahawa Cafe&Restaurant, huu mvinyo nitaenda kusheherekea na wanzangu kambini”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.