Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya wakimdhibiti mchezaji wa Uganda
Tetesi

Beki Yanga Mambo Safi Kuvuna Hela ya Usajili

Sambaza....

Mlinzi wa kati wa Klabu ya Yanga ni kama neema inaendelea kumuangukia kwani viongozi wake tayari wamemuita tena mezani ili kumuongezea mkataba wakuendelea kuhudumu Jangwani kwa Wananchi.

Ibrahim Bacca aliyejiunga na Yanga akitokea KMKM ya Zanzibar baada ya kufanya vyema na kumvutia kocha wa Yanga Nasradine Nabi sasa yupo mezani na viongozi wa Yanga akitakiwa kuongeza miaka mingine miwili ya kuwepo hapo.

Mkataba wa Bacca na Yanga unamalizika mapema January mwakani lakini Yanga wanataka kumuongezea mwingine ambao utamuweka hapo mpaka mwaka 2026 huku pia wakimuongezea mshahara zaidi wa anaoupata sasa.

Ibrahim Hamad Bacca.

Mlinzi huyo ambae amepenya mpaka kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania  “Taifa Stars” amekua sehemu muhimu ya kikosi cha Yanga haswa kipindi hiki ambacho Yanga imekua na ratiba ngumu ikishiriki michuano mingi ya nje na ndani ya nchi.

Bacca amekua nguzo muhimu katika kuanzisha mashambulizi kutokea chini lakini kwa kiasi kikubwa amekua akicheza mipira ya juu kwa ustadi mkubwa na kupelekea Yanga kupunguza kufungwa magoli ya aina hiyo akiwepo uwanjani.

Sambaza....