Brazil baada ya kutwaa kombe la Dunia 2002.
Kombe la Dunia

Brazil na maajabu ya herufi “R”

Sambaza....

Wapwa nawakukumbusha tu kila kilichokuwa na mwanzo kina mwisho. Unakikumbuka kizazi cha’ R ‘ cha Brazil kilichotwaa ubingwa wa kombe la Dunia 2002?

Baada ya kukosa ubingwa mwaka 1998 kwa fainali nzuri ya kupendeza kati yao Brazil na Ufaransa.

Brazil walirejea kwenye michuano ya mwaka 2002 kivingine kabisa hawakutaka kufanya kosa tena kama ilivyokuwa kwa fainali ya mwaka 1998.

Kwa mujibu wa tafiti kocha mwenye wakati mgumu katika kuteua timu ya Taifa duniani basi ni kocha wa Brazil kwa kuwa ina idadi kubwa sana ya watu, nchi hiyo ina watu zaidi ya milioni 200.

Hivyo kwa wastani huo kupata wachezaji wenye uwezo mkubwa hawawezi kupungua 5000-10000 wenye ‘viwango vya lami’.

Rivaldo.

Hivyo basi inapokuja suala la kuchangua wawakilishi 23 waiwakilishe nchi ni mbinde haswa ukiachilia ufundi au kipaji cha mchezaji lazima pia bahati itawale na ndiyo maana wao wanaite timu yao ‘Selecao ‘ kwa maana ya ‘wateule’.

Ukiangalia mafanikio ya Brazil kwenye kikosi chao cha mwaka 2002 kulikuwa na wachezaji 8 ambao majina yao yanaanza na R hivyo huwa tunaita kizazi cha “R”.

Ronaldinho.

Kulikuwa na Rogerio Ceni, Robert Carlos da Salva, Roque Junior, Ricadinho, Ricardo Kaka ,Ronaldo di Lima, Rivaldo na Ronaldinho aliyechukua nafasi ya Romario kwenye uteuzi wa mwisho.

Sijui kulikuwa na siri gani kwenye herufi hiyo maana tangu hapo hawajawahi kutwaa tena ubingwa ndani ya fainali 4 za Kombe la Dunia sijui kama itakuwa zamu yao 2022 pale Qatar.

 

Sambaza....