Wachezaji wa Simba wakishangilia mbele ya mashabiki wao
Mabingwa Afrika

CAF yakubali rekodi ya Simba Ligi ya mabingwa

Sambaza kwa marafiki....

Shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF limeonyesha kuikubali rekodi ya Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa na kuthibisha ndio baba lao katika kupindua matokea.

Ipo hivi mwaka 1979 Simba ilicheza na Mufulira Wonderers ya Zambia jijini Dar es salaam katika mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya mabingwa. Simba ilikubali kichapo cha mabao manne kwa sifuri, lakini katika mchezo wa ugenini Simba ilikwenda Zambia na kupindua matokeo matokea nakushinda mabao matano kwa sifuri.

Katika ukurasa rasmi wa CAF wa instagram Caf online wametupia mchezo huo huku wakisema ni Simba pekee ndio wanaoshikilia rekodi hiyo ya “Comeback” ya nguvu mpaka sasa katika michuano hiyo.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.