Chico Ushindi
Uhamisho

Chico safari imemkuta, Yacouba ngoma ngumu!

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara leo amethibitisha klabu yake ya Yanga itabaki na wachezaji kumi na mbili pekee wakigeni na si kumi na nne waliopo sasa.

Yanga baada ya kuongeza wachezaji watano wakigeni katika usajili msimu huu imejikuta ikiwa na wachezaji kumi na nne wakigeni hivyo kuhitajika kupunguza wawili ili kuendana na kanuni.

Yacouba Sogne na Yusuph Athuman.

Manara akizungumza na waandishi wa habari leo amesema wao hawataenda “pre season” wakifanya mchujo bali watawaacha wachezaji wawili ili wabaki kumi na mbili.

“Tumekubaliana na walimu pamoja na wenzetu TP Mazembe kumrudisha Chico Mazembe, hivyo msimu ujao hatutakua nae atarejea Congo katika klabu yake,” Haji Manara.

Fiston Mayele (9) na Chico Ushindi (25)

Pia Haji alizungumzia hali ya mshambuliaji wao Yacouba Sogne baada yakupona majeraha yake na mustakabali wake katika kikosi.
“Yacouba tunasubiri arudi tutazungumza nae, baada ya majeraha bado hajawa fiti kwa asilimia 100 hivyo akija tutazungumza nae tuone ni kwa jinsi gani tutaachana nae.” Haji Manara

Baada ya usajili wa Joyce Romalisa, Benard Morrison, Lazarious Kambole, Aziz Ki na Gael Bigirimana sasa Yanga itakua na wachezaji kumi na nne wakigeni wakiungana na wale waliokuepo msimu ulimalizika


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.