Stori

CRDB Bank na Simba ni Unyama Mwingi

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba leo imeingia makubaliano na benki inayosikiliza “The Bank that listen” CRDB katika kutoa kadi za mashabiki.

Katika shughuli hiyo ya kutangaza makubaliano hayo iliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club ilishuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Spika Mussa Hassan Zungu, Mtendaji mkuu wa CRDB Abdulmajid Nsekela, Faris Seif mkuu wa kitengo cha kadi, Mwenyekiti wa bodi ya Simba Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Simba Murtazar Mangungu.

Katika hafla hiyo iliyofana Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Imani Kajula alisema “Leo tunashuhudia ushabiki wenye faida, mashabiki wa klabu ya Simba watapata fursa nzuri ya kupata kadi za CRDB huku wakiwa wanaishabikia timu yao,” alisema na kuongeza

“Kutakua na kadi maalum za watoto ambazo zitasimamiwa na wazazi wao, kadi za Platinum, akaunti ya Simba na kadi za mashabaki wa Simba pia.”

Imani Kajula, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba.

“Pia kwa mashabiki wetu wanawake kutakua na Simba Queen akaunti ambayo itakua na bima pia, kadi za watoto ambazo zitawawezesha kuingia bure katika matamasha ya Simba na kule uwanja wa Bunju,”  Kajula.

Pia mtendaji mkuu wa CRDB Benki Abdulmajid Nsekela alielezea mapenzi ya benki ya CRDB katika soka na jinsi ambavyo wateja naashabiki wa CRDB na Simba watakavyofaidika.

“CRDB sisi ni waumini wakubwa katika teknolojia na mpira, hivyo tunawapa mashabiki wa Simba kuona umuhimu wa kuishabikia timu yao. Sisi ndio wakongwe wa masuala ya kadi nchini na ndio maana leo tunashirikiana na Simba.”

Mtendaji mkuu wa Benki ya CRDB Abdulamajid Nsekela.

“Simba ni klabu kubwa iliyoleta heshima katika nchi hii, nawapongeza wachezaji na viongozi kwa kazi nzuri waliyoifanya. Nasisi CRDB tutakua bega kwa bega nanyinyi katika safari ya mafanikio.”

Nae Salim Abdallah mwenyekiti wa bodi ya Simba alimalizia “Nawashukuru CRDB kwa kuingia makubaliano na klabu bora nchini (namba 7 kwa ubora Afrika) kwa maana mmeona Simba ni sehemu sahihi.

Kwa kuuona ukubwa wa CRDB na sisi Simba na ndio maana halikuishia ofisini tu, tukaamua kuja hapa. Niwahakikishieni mwaka huu unyama utakua mwingi.”

Mwenyekiti wa bodi ya klabu ya Simba Salim Abdallah “Try Again”.

Benki hiyo ambayo pia ipo nje ya mipaka ya Tanzania pia inafanya shughuli zake katika nchi za Burundi na Congo DRC. Kwa hapa nchini Crdb ina atm zaidi ya 500, matawi zaidi ya 256, mawakala 30,000 na sehemu za kufanya malipo 5000.

Sambaza....