Uhamisho

Donald Ngoma atemwa na Azam Fc

Sambaza....

Aliyewahi kuwa mshambuliaji Yanga , Donald Ngoma ambaye kwa kipindi hiki alikuwa kwenye timu ya Azam FC ameachana na klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi , Mbagala jijini Dar es Salaam.

 

Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti tangu akiwa Yanga , Azam FC walimsajili akiwa na majeraha ya goti kisha wakaanza kumtibu kwa kumpeleka Afrika Kusini kwa matitabu zaidi.

Alifanikiwa kupona lakini aliporudi uwanjani hakuwa kwenye kiwango kile kikubwa ambacho alikuwa nacho kipindi ambacho yuko na Yanga ambao alifika nao robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mkataba wake na Azam FC umemalizika mwezi huu na Azam FC wameona hawawezi kuendelea naye tena , hivo pande zote mbili zimekubaliana kuachana hivo Donald Ngoma kutokuwa mchezaji wa Azam FC tena.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.