Blog

Eto’o anamfuatilia Kelvin John.

Sambaza....


Samuel Eto’o mchezaji nyota na mfanyabiashara kutoka nchini Cameroon, ambaye amewahi kuwika katika vilabu kadhaa barani Ulaya alikuwa akimfuatilia Kelvin John. Eto’o aliyewahi pia kuchezea Real Madrid mwaka 1997–2000, nabaadae kuichezea kwa mfanikio FC Barcelona, aligundua kipaji ambacho Kelvin anacho.

Katika mahojiano ambayo tunaendelea kukuletea baina yetu na Kelvin, ametuambia stori yake baada ya kukutana na Eto’o nchini Ufaransa. Tukataka pia kujua ni ‘nondo’ gani Eto’o alimkabidhi pia.

Huku akionekana kuchangamka kidogo Kelvin John alianza kwa kusema “Kitu cha kwanza ambacho aliniambia, kuwa hajawahi kuniona ila akaniahidi kuwa atanifuatilia kwenye mashindano ya Afcon.”

Tanzania vs Uganda wakati wa AFCON U17

“Alianza kunifuatilia, nakumbuka kwenye mechi dhidi ya Rwanda alinifuatilia alioneshwa video yangu” Wakati huo Serengeti boys ilikuwa nchini Rwanda kwaajili ya michuano ambayo timu iliaikwa.

Lakini haikuishia hapo tu, kwani baado alihakikishiwa kuendelea kufuatiliwa katika michuano mikubwa ya AFCON U17 “Kitu alichokisema, ni niongeze bidii na akaniahidi kunifuatilia kwenye mashindano ya Afcon”

Mambo yalikuwa tofauti kidogo katika mashindano ya AFCON U17 baada ya Kelvin kuahidiwa kutafutiwa timu Ufaransa, timu haikufanya vizuri “Aliniahidi kama nikifanya vizuri atanipa ofa ya kwenda timu yoyote kubwa nchini Ufaransa” aliongeza Kelvin.

Tovuti ya kandanda.co.tz kwa wiki hii yote itakuletea mahojiano ambayo imefanya na Kelvin John, mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys). Fuatilia mfululizo wa mahojiano hayo kwa njia ya uchambuzi pekee hapa hapa katika ulimwengu wa soka, ukiletwa na mimiMartin Kiyumbi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.