Feisal Salum
Blog

Feisal Salum fanya hivi uondoke Yanga!

Sambaza....

Nilipokuona kwa Mara ya kwanza kwenye viwanja vya Maisala kule Zanzibar miaka 8 hivi nyuma nilijisemea nafsini mwangu “haka katoto kanajua Mpira”. Hakika sikuidanganya nafsi yangu hasa nilipokuja kukuona tena kwenye mashindano ya Cecafa pale Kenya 2017 nikaisemea nafsini sikuidanganya Akili yangu.

Kama mvulana huyu nilivyoangalia kwa jicho la “scout” miaka kadhaa nyuma, leo kafika kuiwakilisha Taifa binafsi ilinipendeza sana, lakini nilifarijika sana pale Amani Stadium mwaka 2018 kwenye kilele cha mashindano ya Mapinduzi Cup. Niliona akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa chipukizi wa Mashindano ambapo pia kulikuwa na kitita cha maana tu ambacho alikipata.

Feisal Salum “Fei toto”

Connection nzuri kucheza Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania ni “platform”, umri wa sasa namuona anastahili kuondoka kwenda nje. Awali alikuwa na matatizo ya kiuchezaji alikuwa yupo “hash”mno kwenye “play style” yake akawa anapata kadi nyingi zisizo na ulazima na kukosa baadhi ya mechi,hili kwa sasa limerekebishika kwa % kubwa.

Alipata bahati ya kuwemo katika kikosi cha wachezaji 23 waliowakilisha nchi katika mashindano ya Afcon ilikuwa platform nyingine yakuonekana zaidi, lakini kwenye mchezo wa kwanza tu dhidi ya Senegal mechi ilikuja kuwa juu ya chipukizi huyu na hata mabadililo yake ilikuwa ya kushindwa kumudu mpambano. Toka pale Fei Toto alipotea kwenye kiwango chake hata alivyorejea kwenye ligi hakuchangamka tena hii inatokana kutokuwa na mtu sahihi wa kumjenga kisaikolojia kwa kile kilichotokea Afcon.

Feisal Salum akitafuta namna ya kumthibiti mchezaji wa Misri.

Lakini Fei wa sasa amereje upya kwenye form yake nadhani ndio muda wa kuondoka sasa, kiufundi anachopaswa kufanya ni kuongeza uwezo wa kutafsiri mahitaji ya mchezo kutokana na muda na tukio (match interpretation) hasa kwenye aina ya pasi.

Kuna muda inahitajika uwapasie washambuliaji kwa pasi sahihi ya toka pale ulipo, lakini kuna muda unapaswa kuwapelekea mpira kwa dribbling ( kukokota ) ama running with a ball ( kupiga Mpira kwa kitambo Fulani na kuufukuzia).

Balama Mapinduzi, Feisal Salum na Haruna Niyonzima wakimuacha mchezaji wa JKT Tanzania.

Zaidi ya hapo ni aina ya Management yako kundi la watu wanaokusimamia kutafuta masoko ya nje kwa wakati huu ukiwa kwenye form kinyume na hapo ukiruhusu miaka 25/26 ikukute hapa hapa itakuwa ngumu kutoka kwenye Ulaya.

Sambaza....