Kombe la Dunia

Vitendo vya ubaguzi vyaiponza Urusi.

Sambaza....

Shirikisho la soka Ulimwenguni (FIFA) limeipiga faini ya zaidi shilingi Milioni 68 Shirikisho la Soka la Russia kutokana na mashabiki wa timu ya Taifa ya Russia kuonesha vitendo vya ubaguzi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ufaransa mwezi Machi mwaka huu.

Katika mchezo huo ambao Ufaransa walishinda kwa mabao 3-1, wachezaji Paul Pogba, Ousmane Dembele na N’Golo Kante wanadaiwa kuwa ndio wahanga wa tukio hilo la kibaguzi.

“FIFA haina uvumilivu kwa vitendo vyovyote vile vinavyoashiria ubaguzi michezoni, kufuatia uchunguzi yakinifu ikiwemo ushahidi wa video, na baada ya uchambuzi wa mambo muhimu ya tukio lile, FIFA imejiridhisha kuwa Russia wameenda kinyume na kanuni ya 58,” Imesema sehemu ya hukumu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Russia ni mwenyeji wa kombe la Dunia ambalo linatarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao, na uwanja wa Krestovsky ambao ulitumika katika mchezo huo wa kirafiki, utatumika kwa baadhi ya michezo ya hatua ya makundi, hatua ya 16 bora, nusu fainali na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu Julai 14, 2018.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x