Tahariri

FIFA wanamtaka Barbara, Simba hawamtaki!

Sambaza....

Jioni, muda ambao tayari nishafanikiwa kugombania seat ya kwenye daladala. Hii ni Dar es Salaam sehemu pekee ambayo hata haki yako unatakiwa kuipata kwa kugombania. Wakati nikiwa nimekaa dirishani, macho yangu yalikutana na mama ambaye mgongoni mwake alikuwa amebeba mtoto mgongoni na kichwani kwake alikuwa amebeba ndizi.

Nafsi yangu ilitamani kuunga mkono biashara yake kwa kununua ndizi lakini kabla sijafanya maamuzi ya mwisho daladala iliondoka kwenye kituo. Sikuwa na nafasi ya mimi kuunga mkono biashara ya yule mama.

Nikiwa bado namtafakari mama yule anayepambana kwa ajili ya mtoto au watoto wake dreva wa daladala aliwasha radio, ilikuwa idhaa ya kiswahili ya BBC, idhaa ambayo tangu utotoni nimekuwa nikiota kufanyia kazi.

Raila Odinga

Masikio yangu yalisikia sauti ya mwanasiasa mkongwe nchini Kenya Raila Odinga akiwa ana mwaga sera zake za kugombea uraisi chini ya mwamvuli wa Azimio akishindana na William Ruto. Hii ni mara ya nne kwa Raila Odinga kugombea uraisi na Kenya na mara zote amekuwa akiangushwa chini.

Wakati natafakari siasa za Kenya, ghafla likaja jina la Wangari Muta Maathai. Mwanamke wa kwanza wa KiAfrika kushinda tunzo ya amani ya Nobel aliyoishinda mwaka 2004. Ngoja nikukumbushe kitu kimoja.

Muta Maatahai.

Kati ya mwaka 1901 hadi mwaka 2018, ni wanawake 52 pekee ambao wameshinda tunzo ya Nobel. Wanaume 852 wamewahi kuchukua tunzo hiyo. Katikati ya watu zaidi ya mia moja kuna mwanamke mmoja hodari kutoka Afrika Mashariki ambaye ana tunzo ya Nobel.

Wakati namtafakari Wangari Muta Maathai jina la Barbara Gonzalenz lilikuja katika akili yangu. Mwanamke mwingine kutoka Afrika Mashariki ambaye amepewa dhamana ya kuiongoza klabu kubwa Afrika Mashariki Simba Sc.

Mwanamke ambaye ameiwesha Simba Sc kufika robo fainali ya ligi mabingwa barani Afrika mara mbili na robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika mara moja. Ndiye mwanamke ambaye anaonesha nia ya kubadilisha mapenzi ya mashabiki wa Simba Sc kuwa pesa ambayo itainufaisha Simba Sc.

Ndiye mwanamke ambaye chini ya uongozi wake ameiwezesha Simba kutia saini mkataba wa utengenezaji na usambazaji wa jezi na kampuni ya Vunje Bei Group kwa dau kubwa la bilioni 2, mkataba ambao haujawahi kutokea kwa upande wa jezi hapa Tanzania.

Ndiye mwanamke ambaye kila uchwao anaongeza wadhamini ndani ya klabu ya Simba. Hakuona Sports Pesa pekee ndiyo wanatosha, akaamua kuwasogeza bodi ya utalii na kampuni ya Emirate Aluminium kama moja ya wadhamini wa klabu hii.

Uendeshwaji huu wa Simba Sc kwa sasa ni uendeshwaji ambao umewasogeza mbali kidogo na klabu hii baadhi ya watu ambao walizoea kuendesha klabu hii kwa mazoea. Hapa ndipo kosa kubwa la Barbara Gonzalen linapoanzia.

Hapa ndipo mwanzo wa mwanamke huyu kuanza kupishana na watu ambao wanaamini wao ni watu wa mpira kuzidi yeye. Watu ambao walizoea kupiga pesa nyingi kupitia tender za jezi , kupitia usajili na ueneshaji wa klabu hii kwa ujumla.

Kuna mianya imezibwa na Barbara Gonzalen ndiyo maana anapata upinzani kutoka kwa watu ambao walizoea kuitumia mianya hii kujinufaisha. Vita hii ya Barbara Gonzalez na watu wanaoijidai ni watu wa mpira ni vita ambayo imekuja kipindi ambacho FIFA imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali ambayo yawatafanya wanawake kujiingiza kwenye mpira.

Barbar Gonzales

Kuna wanawake ambao hawawezi kucheza mpira lakini wanatengenezewa mazingira ya kuuongoza mpira, kuwa waamuzi kwenye mpira, kuwa madaktari, wana sheria na mawakala wa mpira wa miguu.

Mwezi wa nne mwaka huu FIFA , UEFA kwa kushirikiana na IMD Business School waliendesha course ya wanawake 32 kutoka mabara sita. Course hii ililenga kuwafundisha wanawake kwenye masuala ya uongozi wa mpira wa miguu, ukocha na kuwapa uwezo wa kujiamini kuwa wanaweza kushiriki vyema kwenye shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu.

FIFA inapambana kila uchwao kuhakikisha wanawake wanashiriki kwa kiasi kikubwa kwenye mpira wa miguu ila Tanzania kuna kundi la watu wa mpira wanapambana kuhakikisha wanawake siyo watu wa mpira wa miguu.

Inawezekana mimba yetu ya mafanikio imetungwa ndani ya tumbo la Barbara kwa ajili ya kuzaa mtoto ambaye atatuokoa kati

Sambaza....