Serie A

Goli linafutwa, Kadi haifutwi.

Sambaza....

Wapwa: Wenye lugha yao wakisema ‘Kuch kuch hota hai’ maana yake ‘kuna kitu kimetokea’ kwa wale wa kwa Malkia (R.I.P) wangesema ‘something happened’

Kuna swali limekuwa likiulizwa sana kwangu iwe DM au kwa njia yeyote ile Kuhusiana na mazingira Ya mchezaji kushangilia goli kwa kuvua jezi wakati alikuwa na kadi ya njano ya kwanza maana yake mwamuzi atampa kadi ya pili ya njano ikiambatana na nyekundu.

Swali la msingi hapa endapo goli litakataliwa kwa kutumia VAR nafasi ya kadi nyekundu ipoje! nayo itafutwa au la hasha.

Niende kwenye majibu ya moja kwa moja kadi haita futwa pale uwanjani utalazimika kutoka nje hata kama goli halitakuwa limehesabika.

Hii imetokea kwenye mchezo wa Juventus na Salernitana , iliyoisha 2-2 mwamba hapo pichani Arkadiusz Milk striker wa Bi Kizee aliingia uwanjani akitokea bench dk 45 wakati huo timu yake ikiwa nyuma bao 2- nyau.

Katika dakika ya 83 alioneshwa kadi ya manjano hadi dk 90 za kawaida ubao ulikuwa unasomeka 2-2 Zikaongwezwa dk kadhaa hivi ilipofika 90+6 alifanikiwa kufunga goli ambalo lingewafanya Juve kuibuka na ushindi wa 3-2 kwa furaha ile kashangilia kwa kuvua jezi.

Kwa kuwa alikuwa na kadi ya njano akaongezea njano ya pili ikiambatana na nyekundu,muda si muda mawasiliano yakafanyika watu wa VAR goli likafutwa Ila yeye binafsi adhabu yake haikufutwa swali hili likawa linajibika moja kwa moja kutoka kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo.


Sambaza....