Ligi Kuu

GSM kujaa na kombe lao.

Sambaza....

Wadhamini wa Yanga sc ambao pia ndio wanaohusika katika kutengeneza na kuuza jezi za Yanga kampuni ya GSM inatarajiwa kuandaa mashindano yao na kutoa zawadi ya kikombe.

GSM Cup inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambapo itazikutanisha Coastal Union ya Tanga dhidi ya Yanga sc.

Wachezaji wa Coastal Union.

Mchezo unatarajiwa kupigwa katikati ya mwezi huu wa nane ambapo itakua ni miongoni mwa maandalizi kwa timu zote mbili kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo ni moja ya makubaliano ya klabu ya Coastal Union na Yanga baada ya Coastal kukubali kuwauzia mlinzi Bakari Mwamunyeto.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.