Fiston Mayele akishangilia na Feisal Salum
Ligi Kuu

Hakuna ‘kitonga’ kwa Yanga leo.

Sambaza....

Panapo majaliwa tunakwenda kuangalia moja ya mchezo mgumu katika ratiba ya ligi kuu ya NBC kwa upande wa Wananchi

Utajiuliza maswali ,kwanini ni mchezo mgumu wakati current form ya Yanga ipo poa sana?

Nami bila ukakasi wowote wala kushinikizwa na mtu yeyote yule nakubalia na form bora aliyonayo Yanga kwa sasa ukifananisha na mpinzani wao wa leo KMC

Katika ligi NBC Yanga amecheza michezo 17 na kushinda 14 kusare 3 na anajumla ya pointi 45 kwenye sehemu ya alama 51wakifunga magoli 29 na kuruhusu 4 tu (hii ni nidhamu kubwa ya ushiriki) inayoleta maana ya kuwa kwenye form

Wapinzani KMC wana alama 22 katika michezo 17 wakishinda 5 tu kutoa sare kadhaa na kupoteza … wapi kwenye nafasi ya 7 ya msimamo wa ligi

Binafsi naiona mechi kwenye ushindani mkubwa kwa sababu ambazo mara nyingi huwa zinawapa faida sana timu hizi kubwa zikutanapo na ndogo hasa zile za mkoani

Nafasi ya kwanza ni Uoga wa timu za mikoani zinapocheza Dar, hofu inayosababisha kupoteza kanuni nyingi za kiufundi mchezoni maana yake ni kuzalisha makosa na kushindwa kuyathibiti

Uzoefu wa wachezaji wengi wa KMC kama Juma Kaseja/Shikalo Hassan Kessy,Dante ,Mateo Ilamfa utawasaidia sana,hakuna woga wameshavitumikia vilabu hivyo vikubwa

Jambo jingine huwa linakuwa ugeni wa uwanja wa Taifa na umati ambao huwa unajitokeza kusupport timu zao hizo unawafanya ‘kuchachawa’

Lakini kwa KMC sitaraji jambo hilo kutokea kwao ,kwa kuwa ni watoto wa mjini kijiografia wanacheza mara kwa mara hapa nk

Kiufundi pia licha ya kupoteza mchezo wao wa mwisho vs Coastal union naona kwamba kikosi chao kimeimarika sana kiufupi wana uhakika wa kupata goli karibu kila mechi toka wamefanya mabadiliko ya benchi la ufundi

Hata pattern ya kucheza unaiona timu imechangamka kwa aina fulani na yupo mchezaji moja moja aliyogain form kama vile Mviyekule ,Kipagwile Aweso nk

Kifupi natarajia kuona upinzani tofauti na ule wa Geita Gold kwenye mechi yake ya mwisho kule Mwanza

Kwa Mayele binafsi atatakiwa kupambana kuanza kutengeneza gap la magoli na Reliant Lusajo ambaye hakufunga katika mchezo ulio pita vs Azam wakiwa wametier 10 kila moja

All the best!

Sambaza....