Ligi Kuu

Hapa Morrison kule Miquissone

Sambaza....

Leo ni siku ya mechi ya ngao ya jamii. Mechi hii imebeba pesa zako. Tembelea https://bit.ly/30LRNGp ili unufaike wikiendi hii.

Moja ya siku ambayo Simba wanatamani kuiona timu yao ikicheza ni leo. Leo wako Arusha wakicheza na Namungo katika mchezo wa ngao ya jamii.

Mchezo ambao umekuja baada ya Simba kucheza na Vital’O ya Burundi kwenye mchezo wa Simba Day na Simba ikaibuka na ushindi wa goli 6-0.

Hassan Dilunga akimgalagaza mchezaji wa Vital’o

Moja ya vitu ambavyo vilivutia katika mechi hiyo ya Simba Day ni uwezo mkubwa wa wachezaji wapya kama kina Ibrahim Ame, Onyango , Lary Bwalya na Bernard Morrison.

Wote walionesha kiwango kikubwa sana kwenye mchezo huu. Kocha wa Simba aliwatumia kwenye mfumo wa 4-3-3.

Mabeki wa nyuma Onyango na Ibrahim Ame ambaye amesajiliwa kutoka Coastal Union walicheza vizuri kwa utulivu huku wakiwa wanaanzisha mashambulizi kutoka nyuma.

Mfumo wa kocha wa Simba unawataka mabeki wa kati kuwa katika ujenzi wa mashambulizi ya timu. Kitu ambacho walifanikiwa sana.

Kwenye eneo la katikati mwa uwanja kulikuwepo na ingizo jipya , Lary Bwalya ambaye alionesha kiwango bora sana. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za kufunga.

Ndemla

Alifanikiwa kutengeneza goli la Bernard Morrison ambaye na yeye ni ingizo jipya katika kikosi cha Simba. Leo hii Simba wanaenda kucheza ngao ya jamii dhidi ya Namungo FC.

Baadhi ya wachezaji ambao hawakuwepo kwenye Simba Day watakuwepo. Mmoja ya wachezaji ambao hawakuwepo ni Luis Miquissone.

Swali kubwa ni namna gani ambavyo kocha wa Simba atakipanga kikosi chake kwa kuwaweka wachezaji wake nyota kwenye kikosi kimoja , Lary Bwalya, Cloatus Chama, Luis Miquissone na Bernard Morrison. Ingekuwa wewe ndiye kocha wa Simba ungepangeje kikosi ?

Sambaza....