EPLMabingwa Ulaya

Herrera aacha ujumbe mzito kwa mashabiki wa Manchester United.

Sambaza....

Kiungo anayeondoka Manchester United Ander Herrera amesema kocha wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer ndiye chaguo sahihi kwa sasa lakini anahitaji muwa wa kuweza kurejea na kuanza kuwania mataji kama ilivyokuwa zamani.

Herrera ambaye anatajwa kuwa atajiunga na Matajiri wa Ufaransa Paris St Germain mwanzoni mwa msimu ujao, amesema anamuamini sana Ole kuwa ndiye mkombozi sahihi licha ya Manchester United kumaliza vibaya msimu huu.

“Nina muamini sana Ole, yeye ni mtu sahihi kwa kazi ile, ninaliamini sana jopo lote la makocha pale United, lakini nafikiri kuna kazi kubwa sana huko mbele, klabu inahitaji muda, hali ya kujiamini na kuungwa mkono na watu wote,” Herrera amesema.

Ikumbukwe kwamba Ole aliichukua Manchester United iliyokuwa chini ya Jose Mourinho Disemba mwaka jana, na aliiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya sita kwenye ligi kuu England, pamoja na kutolewa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Barcelona.

Licha kuanza vizuri kwa kushinda michezo 10 kati ya 11 toka achukue mahala pa Jose Mourihno lakini Ole amemaliza vibaya, kwani katika michezo 12 iliyopita amefanikiwa kushinda michezo miwili pekee huku wakimaliza msimu kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Cardiff jumapili iliyopita.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.