Ligi Kuu

Hii ndio Yanga bwanaa…

Sambaza....

Baada ya kutua na ndege saa tano asubuhi Jijini Dar es salaam wakitokea Mbeya katika mchezo wa Ligi walipokabidhiwa kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC walilakiwa na mashabiki wao waliokua wanawasubiri kwa hamu.

Baada ya kutoka uwanja wa ndege wachezaji walipanda gari maalum na kuanza kupitia barabara za Tazara, Kamata, Msimbazi, Jangwani na Samora.

Tazama hapa “vibe” la Wananchi jana lilivyokua:

Wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye gari maalum wakipita mitaani ya Msimbazi Jijini Dar es salaam.
Wananchi waliojitokeza kupokea kombe lao katika Kijazi Fly over.
Wananchi walikitokeza kila kona.
Shangwe la ubingwa likafika mpaka Salamander Tower makao makuu ya mfadhili mkuu wa Yanga GSM
Afrika ilitikisika na makocha wakubwa Afrika walituma pongezi zao kwenda kwa Wananchi!

Yanga imetwaa ubingwa wa 28 wa Ligi Kuu Bara na mpaka sasa haijafungwa hata mchezo mmoja.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.