Blog

Hiki ndicho kilichokwamisha Ajibu kwenda Mazembe

Sambaza....

Taarifa ambazo tovuti yetu imezipata ni kwamba kilichomkwamisha Ajibu kwenda TP Mazembe ni biashara ambayo imefanywa kati ya Ajibu na Simba kabla ya ofa ya TP Mazembe kutua mezani kwa klabu ya Yanga.

Kwa habari chini ya kapeti ni kwamba Ibrahim Ajibu alikwishapokea kiasi cha milioni 77 kutoka kwa klabu ya Simba tangu mwezi Aprili, na ofa ya TP Mazembe ilikuja na Milioni 57.5 (Dola 25,000). Hivyo kwa hesabu hii, biashara hii isingefanyika maana muuzaji kivuli angekuwa amepata hasara.

Hivyo, huenda Ajibu kwa upande fulani hana makosa kusababisha mazunngumzo yashindwe, au la alitakiwa arudishe 77 ili afanye biashara ya 57, kwa kuangalia zaidi nini kilicho mbele.

Mkurugenzi Mtendaji wa Simba SC, Bwana Magoli ameiambia tovuti hii kuwa Ajibu si mchezaji wa Simba  hivyo haihusiki na biashara hii, nna alipoulizwa kuhusu tetesi za kuwa Ajibu kasaini Simba hakuweza kutujibu chochote.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.