Mataifa Afrika

Huyu Nyoni ni habari nyingine, Tungeendaje kuwavaa Uganda bila yeye?

Sambaza kwa marafiki....

Simba sports club jana iliweka historia nyingine kwa kufuzu kwenda hatua ya nane bora yaaani robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Africa pongezi nyingi saana ziende kwao.

Lakini kuna jambo la kujifunza kuelekea mechi yetu ya mwisho kugombania kufuzu Africon 2019 ukiachilia mbali moyo wa kupambana kwa wachezaji dakika zote 90 na nguvu ya mashabiki,Huyu Erasto Edward Nyoni ni vizuri kaitwa sasa kujiunga na Timu ya Taifa akichukua nafasi ya Vicent Dante.

Hivi ni nani ambaye alikumbuka kwamba Erasto Nyoni katokea majeruhi? Tena majeruhi ya zaidi ya mwezi mmoja? Yawezekana watu tumesahau kabisa kwamba mechi ya jana ilikuwa zaidi ya fainali,kwangu mimi huyu Erasto Nyoni ndie alie kuwa shujaa wa kweli ndipo afate kocha Aussems Uchebe na Niyonzima.

Safu ya ulinzi ya Simba ilionekana kutulia sana na kupunguza kwa asilimia kubwa saana yale makosa yaliowagharimu kule Kinshasa na Misri,makosa aliyokuwa anayafanya Mo Hussein hasa akipanda kushambulia hayakuonekana kabisa sababu Nyoni alikuwa mwepesi kuziba pengoWawa alipoenda kumsaidia Zana pembeni Katikati hapakuonekana kabisa pengo,huyo ndio Nyoni.

Kwake Nyoni ukubwa na umuhimu wa mechi wala hauku husiana kabisa na mechi fitness,kama hujui kuwa Nyoni alikuwa majeruhi baasi huwezi fikiria hata kidogo kwamba mwanaume huyo mara ya mwisho kucheza mechi ya ushindani ilikuwa mwezi wa kwanza kwenye mapinduzi cup.

Ngoja nikurudishe nyuma kidogo Timu ya Taifa ya Tanzani mwaka jana ilipocheza mechi bila Erasto Nyoni kulee Cape Verde na kufungwa goli 3 kila mtu alilalamika kuwa hajawahi kuona safu mbovu ya ulinzi kama ile,kilio kiliposikika Nyoni akaitwa kwenye mechi ya marudiano Dar ikiwa na safu ile ile akaongeza tu Nyoni mambo yalibadilika kabisa kana kwamba imebadilishwa safu nzima ya ulinzi.

Nyoni uwanjani ni kiongozi lakini pia anauweze kuukanyaga kadumu kwenye kiwango chake kwa zaidi ya miaka kumi huyu ni kama Sergio Ramosi pale madrid akiwa hayupo lazima ujue hayupo.

Timu yetu ya Taifa itakuwa na mchezo mgumu saaana siku ya jumapili ijayo dhidi ya Uganda mchezo ambao ni mgumu na wa lazima kushinda kwetu yaani punda afe mzigo ufuke, Amunike ametumia  busara sana kumuita tena Nyoni baada ya hapo kabla kuwa alikuwa majeruhi na sasa wote tumeona kuwa kapona  na Amunike amefanya kitu cha maana sana kumuongeza ili akasaidiane na kina Yondani pale nyuma. Ingawa amechukua nafasi ya Vicent Dante, lakini hakika hii ni nafasi yake muhimu sana.

Mechi dhidi ya Uganda ni mechi ya kwenda kupambana sio kujenga kikosi yaani ilipaswa hata kama Yondani yupo gerezani basi tukaombe ruhusa kwa Rais ili akapambanie nchi kama ambavyo Uganda hufanya kwa Jurko Mushird hata kama kakosa namba Simba lakini timu ya taifa yupo first eleven tena kwa kiwango boura kabisa.

Nyoni kuna funzo katupa jana kwa kiwango chake kazi kwetu kuamua kujifunza au kujifanya hatujaona kitu tukumbuke shukakumekucha. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Stars#TukutaneAfricon2019.

-Zamoyoni Mbwale

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.