Mashindano

Infantino kuwasilisha mapendekezo mawili katika mkutano wa FIFA ijumaa hii mjini Kigali.

Sambaza....

Rais wa Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni (FIFA) Gianni Infantino amepanga kupeleka agenda za kuanzisha mashindano mawili ya kimataifa katika mkutano wa FIFA utakaofanyika Ijumaa ya wiki hii.

Mkutano huo wa FIFA unatarajiwa kufanyika mjini Kigali nchini Rwanda Ijumaa hii na haijajulikana kama agenda hizo mbili za kupendekeza kuanzisha mashindano makubwa ya Kimataifa itapigiwa kura ama laa na wajumbe wa FIFA.

Mwezi Mei mwaka huu Infantino alipendekezwa kuanzishwa kwa mashindano madogo ya kombe la dunia (Min World Cup) ambayo yangekuwa mbadala wa michuano ya kombe la Mabara inayofanyika kila baada ya miaka minne.

Katika pendekezo lake alisema kwamba yapo makampuni makubwa ambayo yapo tayari kutoa Dola Bilioni 25 kudhamini mashindano hayo kwa miaka 12 kuanzia mwaka 2021, kampuni kubwa la SoftBank Group la nchini Japan likitajwa zaidi kuchukua tenda hiyo.

Pendekezo la Gianni Infantino linaanisha kuwa kuwepo kwa mashindano mawili makubwa ya dunia la kwanza ni Kombe dogo Dunia litakaloshirikisha jumla ya timu nane za Taifa kwa kipindi cha kila baada ya miaka miwili tofauti na ile michuano ya kombe la Mabara inayoshirikisha timu nane kwa kila baada ya miaka minne.

Pendekezo hilo linataja kwamba michuano hiyo itafanyika kati ya mwezi Oktoba au Novemba ya kila mwaka usiogawanyika kwa mbili kuanzia mwaka 2021 na kwa mantiki hiyo kombe la Mabara litafutwa.

Pendekezo la pili ambalo Infantino anapanga kuliwasilisha katika mkutano huo wa FIFA ni kuongeza timu katika michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu kutoka timu saba hadi timu 24 na litafanyika kila baada ya miaka minne.

Ikumbukwe kwamba michuano hiyo inafanyika kila mwaka katika mwezi Disemba ambapo mabingwa wa vilabu katika mabara saba hukutana na kucheza michuano midogo ili kupata bingwa wa Dunia.

Mapendekezo haya yanaweza kupata upinzani mkali kutoka kwa mashirikisho ya soka ya Ulaya yakiongozwa na Rais wa UEFA Aleksander Ceferin.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x